Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huu Ndiyo Ukweli Wa Asili

Asili huwa ina upacha kwenye kila kitu. Ndiyo maana tuna asubuhi na jioni. Tuna usiku na mchana.

Kwenye zuri kuna baya. Upacha wa kila jambo lolote lile, ni la kwetu na siyo la mtu mwingine.

Binadamu huwa tunapenda kufikiri kuwa sisi mazuri ndiyo ya kwetu na mabaya si ya kwetu. Hapana. Mabaya na mazuri ni ya kwetu pia. Yako katika sehemu ya maisha yetu.

Tunapojiandaa kwa mazuri tunapaswa kufikiria pia upacha wa mazuri ni mabaya.

Kila siku jiandae kiakili kukutana na kinyume cha kile ulichonacho.

Vyote ulivyo na wote unaohusiana nao umeazimwa kwa muda na ipo siku vitu vyote na wote unaohusiana nao watarudi kwao. Na inapotokea hivyo, tujikumbushe kuwa asili imefanya kazi yake na sisi hatowezi kufanya chochote.

Mtakatifu mmoja aliwahi kusema, “Mungu wangu na yote yangu”
Kumbe basi, tunaalikwa kushukuru kwa yote. Tunapokuwa na mazuri tukumbukwe kuwa ipo siku tutakuwa na kinyume chake.

Hatuna udhibiti wa vitu vitu vyote hapa duniani. Vitu vingine viko nje ya uwezo wetu.

Ukitaka uumie sana kwenye haya maisha jaribu kwenda kinyume na asili. Ukitaka ufurahie jifunze kuishi kadiri ya sheria ya asili.

Asili huwa haina ubaya ila mitazamo yetu juu ya asili ndiyo mibaya.

Hatua ya kuchukua leo; jifunze kuyapokea yote kwani yote ni yako.

Jifunze kutumia vizuri kile ulichonacho kabla hakijaondoka. Thamini kila kitu ili hata siku kikiondoka hutoumia sana kama yule aliyekuwa anachukulia poa mambo.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: