Design a site like this with WordPress.com
Get started

Maswali Mawili Ya Kujiuliza Kila Siku Asubuhi Na Jioni

Hakuna anayeamka asubuhi na kupanga kuwa na siku ya hovyo. Kila mmoja wetu anapenda kuwa na siku bora na ndiyo lengo la kila m

Ili uweze kuimiliki siku yako lazima uweke mipango ya kumiliki siku yako. Usipojiandaa kuimiliki siku utakuja kumilikiwa.

Usipojiandaa kutawala, utatawaliwa. Usipojiandaa kushinda, utashindwa. Jiandae kupata kile unachotaka na siyo vinginevyo.

Hapa nimekuandalia maswali mawili yatakayochochea wewe kuwa na siku bora sana.

Wakati wa asubuhi kabla hujaanza siku yako, jiulize, je, ni mambo gani mazuri nakwenda kufanya leo?
What good shall I do today?

Unapoamka asubuhi fikiria kufanya mazuri. Na tena jiulize kabisa leo ninakwenda kuacha alama gani kwa watu? Naenda kufanya mazuri kiasi gani?

Kila mmoja wetu anayo mazuri ndani yake. Fikiria namna ya kutenda mema na nenda kayatende hayo kwa vitendo.

Baada ya kufanya kazi zako zote za siku, kabla ya kulala jioni tenga muda wa kuwa na tafakari binafsi. Jiulize, je, ni mambo gani mazuri uliyofanya ndani ya siku yako?
What good have I done today

Hapo unakuwa unapima kile ulichofanya asubuhi. Unakuwa unajifanyia tathimini binafsi. Asubuhi ulijiambia unakwenda kufanya mazuri gani sasa jioni unapata muda wa kutafakari yale mazuri uliyofanya.

Unapata nguvu pale unapofanya mazuri. Mazuri yanakupa hamasa ya kuendelea mbele. Hamasa ya kuthubutu kufanya zaidi.

Hatua ya kuchukua leo;
Kila siku asubuhi, jikumbushe ni mambo gani mazuri unakwenda kufanya leo.

Kila siku jioni, tafakari ni mambo gani mazuri uliyofanya ndani ya siku yako.

Ni vema sana ukiwa unaandika yale unayopata pale unapotafakari yote hayo.

Ukiwa unafanya kila siku, utajijengea utamaduni mzuri utakaokupa faida kwako mwenyewe na kwa wengine pia.

Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi ajiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com //

Asante Sana
©Kessy Deo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: