Changamoto moja ambayo tunayo sisi binadamu pale tunapopata fedha ni matumizi makubwa ya fedha kuongeza bila hata ya kutegemea.
Kuna kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka. Sasa hapa usipokuwa makini na fedha zako utajikuta huna hatua unayopiga, ulikuwa unaishi katika kipato fulani lakini kipato kikiongezeka tu mtu anashindwa tena kuishi kadiri ya kipato alichokuwa nacho mwanzo.
Kuwa makini, unapoongeza kipato usiongeze matumizi ishi kawaida tu kama ulivyokuwa unaishi hapo awali.
Leo nakualika kitu kimoja rafiki yangu kwenye suala la fedha ambacho ni jifunze kuishi kwa kile ulichonacho. Usipende kuishi kwa kile ambacho huna, kwani hapa lazima utajikuta umeingia kwenye madeni.
Jifunze kuishi kwa kile ulichonacho itakusaidia kupata fedha za kuwekeza, kufanya maendeleo na nk. Lakini pia itakusaidia kuwa na amani kwa sababu unaishi kwa kile ambacho unacho na siyo vinginevyo.
Usinunue kwa sababu una fedha ya kununua.
Usiishi juu ya kipato chako hata kama kipato chako ni kikubwa sana. Ishi chini ya kipato chako itakusaidia kuwa na fedha za kuwekeza kwenye mambo ya maendeleo.
Hatua ya kuchukua leo; jifunze kuishi kwa kile ulichonacho. Hata ukipata kikubwa usiongeze matumizi , endelea kuishi kwa kile ulichonacho.
Kwahiyo, matumizi makubwa huwa tunayataka sisi wenyewe, tukiona tuna fedha basi tunataka kununua hata kama siyo muhimu.
Tujifunze kuishi kwa kile tulichonacho.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo
Asante kwa mafundisho ninajifunza kila siku kitu kipya
LikeLike
Karibu sana Catherine
LikeLike