Hakuna kitu kimoja peke yake kinachoweza kuifanya ndoa kuwa bora, ndoa inajengwa na misingi ya vitu mbalimbali. Ni kama vile ambavyo hakuna mtu ambaye anaweza kusimama peke yake kwa kila kitu bila kuwategemea wengine.
Viko vitu vingi ambavyo vikikosekana katika ndoa lazima kutaibuka changamoto ya kila aina na mimi leo nakwenda kukuambia kitu ambacho kinasababisha ndoa nyingi kuwa na changamoto za kila aina endapo kitu hiko kitakosekana.
Fedha ikikosekahna katika ndoa yoyote ile inaibua kila aina ya changamoto katika maisha ya ndoa. Angalia matatizo au ugomvi mkubwa unaotokea katika ndoa nyingi chanzo chake kikubwa ni fedha.
Kama fedha iko katika ndoa, wana ndoa wanakuwa huru kufanya kile wanachotaka lakini fedha ikikosekana katika ndoa wanandoa watashindwa kupata kile wanachotaka na hapo ndipo changamoto zinapoibuka.
Hakuna wito ambao unaweza ukauchagua ukaenda vizuri bila kuwa na fedha. Licha ya kuwa kila mmoja wetu yuko katika wito aliochagua lakini kila wito unahitaji fedha ili uweze kwenda vizuri. Kwa mfano, wito wa ndoa unahitaji fedha ili uweze kulipa bili mbalimbali na pale fedha zinapokosekana za kulipia bili mbalimbali za kifamilia ndiyo kila aina ya changamoto zinaibuka hapo.
Fedha zinapunguza changamoto ndogo ndogo katika ndoa na kupelekea wanandoa kutokua na kero za kijingajinga.
Baada ya kuona kuwa fedha ni muhimu sana kwenye ndoa basi tunaalikwa kuwa na fedha katika ndoa zetu.
Mume au mke hakikisha unapambana kukusanya fedha nyingi ili basi ndoa yenu iwe na uhuru wa kifedha muweze kupata kile mnachotaka.
Ndoa nyingi bado hazina uhuru wa kifedha na dalili ya kwanza ya kuthibitisha hili ni pale mnapokuwa mnahitaji kitu halafu hamna hela, tungekua na fedha tungefanya moja, mbili, tatu lakini ukiwa na fedha unakuwa kile unachotaka.
Huwezi kupata kile unachotaka kama huna fedha za kukuwezesha kupata kile unachotaka.
Muda mwingine hata upendo, amani, furaha huwa inakosekana pale ndoa inapokuwa haina fedha za kujiendesha, kama ndoa ni taasisi sasa nioneshe taasisi inayoweza kujiendesha bila fedha nami nitakuonesha taasisi iliyokufa.
Hatua ya kuchukua leo; Kila mwanandoa aelewe kuwa fedha ni kitu kizuri katika ndoa hivyo unatakiwa kujituma ili ndoa yako iwe na fedha. Fedha inapokosekana katika ndoa maovu na changamoto za kila aina.
Kwahiyo, fedha haiwezi kumaliza changamoto za ndoa lakini fedha ikiwepo kwenye ndoa inapunguza changamoto na mambo mengi yanakwenda vizuri.
Muhimu;
kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com //, kessy@ustoa.or.tz
Asante Sana
©Kessy Deo