Watu wengi wanaweza kujiuliza je nina wezaje kuwa na hekima? Hili ndiyo swali ambalo linaulizwa na watu wengi.
Iko njia rahisi ya kuweza kuwa na hekima katika maisha yetu nayo ni kutumia akili. Kwa kuwa sisi ni binadamu tulioumbwa kwa jinsi ya ajabu tumepewa akili kubwa ya kuweza kujua zuri na baya.
Kwa kutumia akili ya kawaida tu tuliyopewa sisi kama binadamu tayari tumekuwa na hekima. Kila mtu akitumia akili yake vizuri basi tayari amekuwa na hekima.
Mbuzi akifunguliwa na kutoka nje ni rahisi kwenda kuvamia mazao ya watu kama yakiwepo, lakini sisi binadamu kwa kutumia akili tunaweza kuchuja zuri na baya.
Kila mmoja wetu anapofanya kosa fulani anajua kabisa hapa nimefanya kosa fulani na kinachokusaidia kutambua hilo ni hekima.
Wewe huwezi ukatoka ndani na kwenda kazini ukiwa hujapiga mswaki au kuvaa nguo, lakini mbuzi yeye atafanya kile anachojua yeye kwa sababu hana utambuzi wowote.
Hatua ya kuchukua leo; tumia akili ya kawaida uliyopewa kuwa na hekima. Chuja kila jambo kabla ya kufanya na kujiuliza je ni sahihi.
Kwahiyo, tumia akili yako kuwa na utambuzi wa mambo mbalimbali, usitumie hisia katika kufanya maamuzi bali tumia akili kufanya maamuzi. Ukitumia akili utakuwa mtu mwenye hekima lakini kwa kutumia hisia utakuwa mpumbavu.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com
Asante Sana