Design a site like this with WordPress.com
Get started

Utaweza Kufika Pale Unakotaka Kama Ukianzia Hapa

Sehemu pekee ambayo huwa inaanzia juu na kwenda chini ni kaburi. Kaburi huwa linachimbwa kwa kuanziwa juu na kufika chini. Mara nyingi mtu yeyote anayetaka kuanza kitu kwa kuanzia juu lazima ataanguka vibaya.

Chukulia kaburi, linaanzia juu na kuelekea chini hivyo basi, hata biashara unatakiwa kuanzia na siyo juu.

Kama unataka kufika mbali basi kubali kuanzia chini, kubali kuanza na kile ulicho nacho.

Watu huwa wanapenda sana kuwa juu lakini hawataki kuanzia chini kwenye mchakato.

Siku zote mtu ukianzia chini kuna faida kwa sababu hata ukianguka hutoumia kama mtu aliyeanzia juu. Pendelea sana kuanzia chini, lakini kuwa na maono makubwa ya kufika kule unakotaka kufika.

Ukianzia chini, chini patakuja kukupa uzoefu utakaokusaidia kufika juu. Pia usidharau vitu vidogo, vitu vidogo ndiyo vina zaa vitu vikubwa.

Kama unataka kufika pale unapotaka, kubali kuanzia chini na kubali kuanza na kile ambacho unacho. Anza na kile kidogo na baadaye kitakufikisha juu.

Usidharau kidogo kwa sababu bila madogo huwezi kuwa na makubwa. Haba na haba hujaza kibaba, hivyo tujitahidi kuweka kazi kwenye kile tunachotaka na dunia itakuwa tayari kutupatia kile tunachotaka.

Kuwa na nia ya kufika kule unakotaka, usione aibu kuanza na mambo madogo madogo, anza nayo yatakusaidia kufika kule unakotaka.

Usisubiri mpaka upate kitu kikubwa sana ndiyo uchukue hatua, bali anza kidogo na mwisho wa siku unakuja kujikuta umemaliza. Ukifikiria safari utaona ni mbali lakini ukianza safari kwa hatua ndogo ndogo utafika tu.

Hatua ya kuchukua leo; anza na kile ambacho unacho na anzia hapo hapo ulipo na utafika kule unakotaka kufika.

Hivyo basi; usipende kuanzia juu, siku zote jifunze kuanzia chini ndiyo uende juu, hata katika hali ya kawaida, mtoto mdogo hawezi kujifunza kuandika kwa kalamu bali anaanzia na penseli na akishaweza na penseli basi ndiyo ataweza kutumia kalamu.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, deogratius kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: