Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hasara Moja Utakayoipata Pale Utakapoianza Siku Yako Bila Kipaumbele

Mpendwa rafiki,

Usipopangilia muda wako vizuri utaishia bila kujua umefanya nini cha maana na huku ukijikuta umechoka.

Ukianza siku yako kwa kutumikia mitandao ya kijamii, bila kujipangilia wewe mwenyewe yale muhimu kwako ni lazima utapoteza siku yako.

Kiufupi rafiki yangu, hasara moja utakayoipata pale utakapoianza siku yako bila kipaumbele ni ;

Kila kitu kitakuwa kipaumbele kwako.

Utaongozwa na matukio na siyo ratiba. Unatakiwa uwe na mwongozo wa siku yako tokea unatokea kitandani mpaka unaporudi kitandani. Kila muda uwe na kitu cha kufanya  usikae tu muda wako ukapotea bila kuwa na kitu cha kufanya. Kama ni kupumzika pumzika kweli na usifanye kitu kingine chochote maana watu wengi hawapumziki kwanini?

Wakipumzika wanafikiria kwenda kufanya kazi na wakiwa kwenye kazi wanafikiria kwenda kupumzika. Uwepo wao unakua haupo kwenye kile wanachofanya kwa muda huo, hivyo wanaishia kutawanya mawazo.

Mwandishi mmoja aliwahi kusema, usipopangilia muda wako vizuri hata shetani ni rahisi kukukamata kwa sababu una upo upo tu. Ukiwa mtu makini hata shetani anakuwa anapata kazi kukujaribu.

SOMA; JINSI YA KULINDA NGUVU ZAKO NA KUWA NA UZALISHAJI BORA

Kutokua ni vipaumbele vyako vya siku ni kama vile mtu ambaye anaishi bila kujua kile anachotaka. Mtu ambaye anaishi bila kujua kile anachotaka ni rahisi kutopata kile anachotaka kwa sababu hajui kile anachotaka.

Hata mtu ambaye anasafiri bila kujua kule anakokwenda hawezi kufika kule anakokwenda kwa sababu hapajui.

Hivyo basi, hatua ya kuchukua leo ni; weka vipau mbele vya siku siku yako. kuwa na orodha ya siku ya yale utakayofanya na usiyotakiwa kufanya. Na ishi kwenye ratiba yako mengine yanayotokea ni kelele kwako achana nayo.

Kwahiyo, ukitaka kupoteza siku yako, ianze bila mpangilio utaishi kuchoka bila kuona kazi kubwa uliyofanya. Kuwa makini na bahili wa muda wako na utafika mbali.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: