Mpendwa rafiki yangu,
Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika zama tunazoishi, zama za mapinduzi ya viwanda kazi za kuajiriwa zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na sasa.
Zama za taarifa zimekuwa na mabadiliko sana, binadamu yuko huru kufanya kile anachotaka yeye.
Dunia inazidi kudhihirisha ukweli kwamba ile hadithi ya nenda shule, soma kwa bidii, faulu na utapata kazi nzuri imeshapitwa na wakati.
Wazazi, mnatakiwa kulifahamu hili, hizi siyo zama za kumkuza mtoto na kumwaminisha katika hadithi hiyo hapo juu.
Ni zama za kumweleza mtoto ukweli wa mambo. Kwa sasa elimu siyo kigezo kikuu cha kupata ajira bali kigezo kikuu ni uwezo wa mtu binafsi.
Vipi kama ukiwa unawafundisha watoto wako kuwajengea uwezo binafsi mapema wa kujitegemea kuliko kuwajengea falsafa ya utegemezi?
Kazi nyingi zinazofanyika katika makampuni mbalimbali , mtu yeyote anaweza kufundishwa na kufanya vizuri ukiondoa zile kazi kama za udaktari, sheria, na kazi nyingine zinazohitaji leseni maalumu ya kuzifanya.
Ushauri huo umepitwa na wakati katika zama hizi, lakini wazazi wengi wamekuwa ni mabingwa na waaminifu kuwaambiwa watoto hadithi hiyo iliyopitwa na wakati.
Badala ya kuwaambia watoto hadithi iliyopitwa na wakati sasa mwambie mtoto wako hadithi hii hapa;
Nenda shule, soma kwa bidii, jijengee ujuzi ambao utakuwezesha kutoa thamani kubwa kwa wengine. kuwa tayari kujituma kwenye chochote unachofanya na utakuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yako, iwe utaajiriwa au utajiajiri mwenyewe.
SOMA; Kitu Cha Kumnyima Mtoto Katika Malezi
Rafiki yangu, ukiwapa watoto wako ushauri huu, utakua umewasaidia sana kwani watakuwa wanajua ukweli wa mambo kwenye hii dunia.
Hatua ya kuchukua leo; wewe kama ni mzazi au mzazi mtarjiwa mwambie hadithi bora mtoto wako ambayo ni hii hapa; Nenda shule, soma kwa bidii, jijengee ujuzi ambao utakuwezesha kutoa thamani kubwa kwa wengine. kuwa tayari kujituma kwenye chochote unachofanya na utakuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yako, iwe utaajiriwa au utajiajiri mwenyewe.
Kwahiyo, wazazi tuachane na nadharia ya nenda shule, soma kwa bidii na utapata kazi nzuri. Badala yake tuwajengee ujuzi ambao utawawezesha kutoa thamani kubwa kwa wengine.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com
Asante sana