Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sala Bora Ya Kuondoa Uvivu Duniani

Uvivu umekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa watu wengi. Watu wamekuwa wanaendesha maisha yao kwa mazoea sana.

Utamaduni wa uvivu huwa unazaa walalamikaji wengi, watu wasipotambua kuwa jukumu la maisha yao ni lao wenyewe watakua wanawalaumu watu wengine kwa wao kuwa hivyo walivyo leo.

Uvivu ndiyo adui mkubwa wa binadamu, watu wanashindwa kuwa na maisha mazuri kwa sababu ya kukosa juhudi katika maisha yao.

Mtu mvivu ni kama kinyesi, kama tunavyojua mtu akijipaka kinyesi hakuna hata mmoja wetu anaweza kumsogelea au kukaa naye. Lazima utamkimbia, sasa na mtu mvivu ndiyo yuko hivyo, hawezi kukaa na mtu bali atakimbiwa.

Hakuna faida yoyote tunayoipata kupitia uvivu zaidi ya hasara. Leo ninakwenda kukushirikisha sala bora duniani ya kuondoa uvivu. Kama wewe uvivu ni sehemu ya maisha yako, basi usiendelee hata kusoma bali ishia hapa hapa lakini kama unauchukia uvivu, karibu tujifunze.

SOMA; Hii Ndiyo Dawa Ya Uvivu

Sala bora ya kuondoa uvivu duniani, ni nidhamu binafsi. Nidhamu binafsi ina nguvu kubwa sana katika maisha yetu.

Ukiwa na nidhamu binafsi, uvivu unakimbia wenyewe. Uvivu na nidhamu binafsi huwa haviwezi kukaa sehemu moja hata siku moja. Ni kama vile paka na panya kuwa marafiki.

Ukatae uvivu kwa kuwa na nidhamu binafsi, nidhamu binafsi ni ile hali ya kujisimamia wewe mwenyewe bila mtu mwingine kukuambia ufanye kitu fulani.

Kwa mfano, tokea tarehe moja octoba mwaka 2016 nilianza kuandika kila siku mpaka leo hii sijawahi kuacha na mwaka huu nimefikisha miaka 3. Sasa kitendo cha kuandika kama hiki ni nidhamu binafsi, sina ambaye ananisimamia bali mimi mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; kama una uvivu katika maisha yako, amua kuwa mtu wa nidhamu binafsi na uvivu utatoweka wenyewe. Kuwa mtu wa kujituma bila kusimamiwa na mtu mwingine.

Kwahiyo, kama unataka kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, Sali sala hii ya nidhamu binafsi. Hakuna mtu mwenye nidhamu binafsi ambaye hajafanikiwa kwenye jambo fulani. Hebu anza kuisali halafu utaniambia matokeo yake.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: