Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usikubali Kufanywa Mtu Wa Namna Hii Kwenye Maisha Yako

Mpendwa rafiki yangu,

Tunatakiwa kufanya kile tunachofanya kwa uaminifu mkubwa sana,kazi unayofanya unatakiwa kuifanya kwa uaminifu mkubwa. Biashara unayofanya unatakiwa kufanya kwa uaminifu mkubwa sana.

Kwenye jambo lolote kwanza huwa anatafutwa mjinga wa kuumizwa au kuuziwa. Angalia makubaliano yoyote yanayofanyika lazima kuna kuwa na mambo haya.

Mmoja lazima akubali kushindwa ili mwingine ashinde, au kila mtu anataka watoke sawa, yaani win to win agreement.  Kuna maeneo ambayo watu huwa wanakubali kushindwa ili waweze kujenga mahusiano fulani na kuwa wengine pia wanakuwa siyo waaminifu wanataka wao washinde tu kwenye kile jambo.

Katika makubaliano yoyote usikubali kufanywa mjinga, wazungu huwa wanasema nani atakuwa samaki mezani, ikiwa ina maana kwamba, kama hakuna mjinga nani atakuwa samaki mezani, yaani nani atakayefanywa kuwa chambo?

SOMA; HII NDIYO AINA BORA YA MAKUBALIANO UNAYOTAKIWA KUFANYA KILA SIKU

Uwe makini sana kwenye kila makubaliano unayofanya na mtu angalia yasiwe yanakuumiza sana , jitahidi usifanywe kuwa mjinga angalau mfikie maamuzi ambayo kila mtu ataondoka na ushindi. Usifanye makubaliano ambayo mtu anakuwa anakunyonya tu. Hakikisha unakuwa na win to win agreement.

Kama hakuna mjinga au samaki mezani basi ujue wewe ndiyo wanataka wakufanye chambo.  Kwenye makubaliano yoyote mnayofanya yaani bargain usikubali kuumizwa, fanyeni kitu ambacho kila mtu ataondoka na amani na siyo mmoja anakuwa mnyonge na mwingine anafurahia ushindi.

Ukitaka uwe unashinda kwenye kila kitu, utakuja kuwaumiza wengine, utaweza kuvunja hata mahusiano na wengine, hivyo siyo kwenye kila jambo ulazimishe ushindi, muda mwingine mpe ushindi hata mteja wako na siyo kumuumiza kila siku. Kwa mfano, kwenye mapatano ya bei ya kitu, kuna watu wanataka faida kubwa, labda wanamuuzia mtu kwa bei kubwa kiasi kwamba upande wa pili unakua unaumia sasa hiyo siyo nzuri.

Hatua ya kuchukua leo; unapofanya makubaliano yoyote yale, usikubali kufanywa chambo, hakikisha kila mnalofanya kila mtu anaondoka na ushindi wake. Siyo upande mmoja ushinde halafu mwingine uumie.

Kwahiyo, unatakiwa kuwa makini, siyo kila mtu ni mzuri kwako, wewe umekuwa kama swala anavyowindwa porini, kila mtu anataka kukuuzia kitu, ukianzia kwenye vyombo vya habari kila siku vinakutaka wewe uchukue hatua ya kununua hivyo kuwa makini sana.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: