Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ushauri Wa Mwanafalsafa Epictetus Kwa Mtu Yeyote Anayetaka Kufanikiwa

Heri ya mwezi agasti rafiki yangu,

Natumaini hujambo na unaendelea vizuri. Niendelee kukutakia kila la heri katika mwezi huu wa nane tunaoanza nao leo. Unaweza kufanya kitu chochote leo na kubadilisha maisha yako.

Zaidi ya miaka elfu mbili mafundisho ya wanafalsafa bado yako hai na yanaendelea kutumika katika jamii yetu. Licha  ya wanafalsafa hawa kuishi miaka ya zamani lakini cha ajabu watu hawa mafundisho yao ndiyo yanahitajika sana katika jamii yetu ya leo.

Watu wengi  hawajui kile wanachotaka katika maisha yao, wengi hawana mpango wa wiki, siku, hawana picha ya miaka mitano au kumi kwenye kile wanachofanya. Tumekuwa ni watu wa kufanya kile ambacho tunakiona mbele yetu lakini siyo kwa mipango sahihi.

Ukitaka kufanya tafiti ndogo, waulize watu je kile wanachofanya wanakipenda, wengi watakuambia hawakipendi. Ni ngumu sana kufanikiwa kwenye kitu ambacho hukipendi lakini utawezaje kufanikiwa kama hujui nini unataka?

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Hand Book of Epictetus( Misingi Muhimu Ya Falsafa Ya Ustoa)

Leo nakupa ushauri wa mwanafalsafa wa ustoa epictetus kwa mtu yeyote yule anayetaka kufanikiwa na hajui wapi kwa kuanzia. Epictetus anasema hivi, kwanza jinenee kile unachotaka kuwa , halafu fanya kile unachopaswa kufanya.

Kama unataka kufanikiwa kwanza jinenee kile unachotaka kuwa. Unatakiwa kujiambia maneno mazuri kila siku unapoamka, kama unataka kuwa tajiri basi jiambie mimi ni tajiri, kama unataka kuwa mwenye bahati jiambie mimi ni mwenye bahati sana kila siku.

Watu wengi hawapendi kujinenea vile wanavyotaka kuwa ndiyo maana hawawi vile wanavyotaka kuwa. Wako ambao kazi yao ni kujikatisha tamaa wao wenyewe badala ya kujitamkia maneno mazuri, wanajitamkia maneno mabaya.

Baada ya kujiambia sasa vile unavyotaka kuwa sasa fanya kile unachopaswa kuwa. Kile ambacho unajinenea kifanye kwa vitendo. Huwezi kujiambia wewe unataka kuwa tajiri halafu huchukui hatua zozote zile. Umekaa tu umeweka mikono mifukoni.

Kama unataka kuwa mtu wa namna fulani hakikisha matendo yako basi yaendane na kile unachotaka kuwa. Haitoshi tu kujinenea bali inahitaji kazi ya nguvu ili kuweza kuwa vile unavyotaka kuwa.

Hatua ya kuchukua leo; kwanza jinenee kile unachotaka kuwa , halafu fanya kile unachopaswa kufanya

Kwahiyo, ili maisha yako yawe mazuri unatakiwa kufanya kazi sana wakati huu, hakuna wakati ambao utaweza kuamka ukiwa umekamilika kila kitu, hivyo unapotaka kuanza wewe anza na ukamilifu haujawahi kuwepo hapa duniani.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, deogratius kessy

0717101505/0767101504

www.mtaalamu.net/kessydeo

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: