Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unajali Wengine Wanasema Nini Kwenye Maisha Yako

Rafiki,

Kila mtu ni kiongozi wa maisha yake.
Hakuna mtu mwingine anayejua zaidi kuhusu wewe kama wewe.

Wewe ndiyo bosi wa maisha yako lakini cha kushangaza wako watu hawajali maisha yao bali wanajali kile wanachosema wengine.

Utakua ni mtu wa ajabu pale unapoacha kujali yako na kujali mambo ambayo hayakuhusu.
Kama wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako kwanini unasikiliza maneno ya watu?

Una kila kitu cha kukufanya uwe na maisha yenye furaha.
Unajua kwanini unajiona maisha yako hayana maana?
Ni pale unapoanza kujilinganisha maisha yako na wengine.

Tunapoanza kujilinganisha na wengine lazima tutaona maisha yetu hayana.
Jikubali na jione wewe ni bora kuliko wengine.
Amini kwenye kile unachofanya na jikubali vile ulivyo

Kuna hasara moja unayoipata pale unapokataa kujikubali,
Unajua ni hasara gani?
Kama wewe hujikubali basi hata wengine hawatakukubali.
Ukijiona wewe huna kasoro na watu watakuchukulia vile unavyojichukulia wewe.

Kama unajali wengine wanasema nini, huwezi kuishi maisha yenye maana, huwezi kuishi maisha unayotaka bali utakua unawafurahisha watu wengine lakini ndani yako unabakia mtu.

Hatua ya kuchukua leo; Ishi maisha yako , usiwaangalie wengine wanasema nini bali angalia kile unachotaka wewe na ishi ndoto yako.

Kwahiyo, kujali ya watu wengine yanasababisha wewe kushindwa kufanya yako.
Kama mtu umejitoa kupambana na maisha yako ,huwezi kufikiria wengine wanasema nini.
Kama unajali wengine wanasema nini maana yake bado hujajua nini hasa unataka kwenye maisha yako.

Kila la heri rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,
Mwl. Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: