Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifahamu Pumzi Ya Biashara Yako

Rafiki,

Biashara ni kama binadamu, inatungwa mimba ( mawazo)inazaliwa ,inakua na hatimaye inakufa.

Biashara ina uhai kama vile binadamu alivyo, kitu chochote kikikosa uhai kitakufa.

Katika biashara nyingi unazoziona zinakufa ujue zimekosa pumzi. Kitu kikikosa pumzi huwa kinakuwa kinakufa.

Leo tutajifunza pumzi ya muhimu katika biashara yako.
Pumzi muhimu ya biashara yako ni mzunguko wa fedha.

Bila mzunguko wa fedha biashara yako haiwezi kukua bali itakufa. Katika hali ya kawaida tu mtu huwezi kuishi bila pumzi maana pumzi ndiyo uhai wenyewe.

Kwenye biashara unayofanya hakikisha ina fedha, ina mzunguko wa fedha. Fedha ni kama damu ya biashara kama ilivyomwili hauwezi kuishi bila damu vivyo hivyo katika biashara haiwezi kwenda bila fedha.

Mzunguko wa fedha ukiwa chanya biashara itaweza kujiendesha vizuri. Lakini mzunguko wa fedha ukiwa hasi biashara inakuwa ngumu kujiendesha yenyewe.

Unatakiwa kukazana kuongeza mauzo kwenye biashara yako ili uwe na mzunguko wa fedha mzuri.

Unapokuwa huna mzunguko chanya kwenye biashara unashindwa kufanya manunuzi pale bidhaa inapokuwa imekwisha au uzalishaji, nk.

Hatua ya kuchukua leo; jiulize leo biashara yako ina pumzi? Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako ukoje ni hasi au chanya?

Kwahiyo, ukitaka kujua kama biashara yako ina mzunguko chanya ni pale ambapo ina uwezo wa kujiendesha yenyewe na unapoona biashara yako haiwezi kujiendesha jua hapo kuna mzunguko hasi.

Kila la heri rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwalimu Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: