Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sababu Mbili Zitakazokufanya Ushindwe au Ushinde Kwenye Jambo Lolote

Mpendwa Rafiki yangu,

Sisi wenyewe huwa tunachangia sana maisha yetu au sisi binafsi kuwa kama tulivyo leo.
Kama ni mafanikio makubwa au hali ngumu kwenye maisha yetu sisi ndiyo tumekuwa chanzo namba moja.

Hadithi ni nyingi sana kwenye maisha yetu. Kila mtu ana hadithi yake ambaye akikuelezea unaweza kujifunza kitu fulani.

Tumepewa uwezo mkubwa na Mungu lakini wengi wetu tunautumia chini ya kiwango.
Huwa hatujiamini kuwa ndani yetu tunaweza kufanya makubwa na mazuri kama wanavyofanya wengine.

Ziko sababu kuu mbili ambazo zinawafanya watu washinde au washindwe kwenye yale wanayofanya.

Sababu kuu moja ya kushinda ni hii hapa
Ni kwanini wewe unaweza.

Hii ndiyo sababu ambayo itakuwezesha wewe ushinde.
Ukianza kujiuliza maswali ya kwanini Mimi ninaweza kufanikiwa katika jambo fulani utaanza kuona nguvu za kwanini unaweza.

Kwanini unaweza ni kama umefungua nguvu za ndiyo ndani YAKO. Nguvu na hamasa kubwa za kuhakikisha unashinda kweli.

Ukitafuta sababu za kushinda utazipata na utaziona nyingi sana.
Kama ulikuwa unaona mambo ni magumu utaanza kuona fursa nyingi zilizokuzunguka ndani yako.

Unataka nini katika maisha yako?
Je umeshajiuliza hata siku moja kwanini unaweza? Ziko sababu za uwezekano kwenye kila unachotaka kuwa.
Kwani ni ndoto gani ambayo wewe unataka kuwa nayo na hakuna mtu ambaye tayari ameshafikia? Wako watu wengi ambao tayari wameshafika kule ambako wewe unataka kufika.

Hivyo basi, sababu ya kwanini unaweza ndiyo itakusaidia uweze kujihamasisha na kushinda kwenye kitu chochote kile.

Sababu nyingine ni kwanini ushindwe.
Ukianza kutafuta sababu za kwanini ushindwe au kwanini huwezi nakuambia hutoweza milele.

Watu wengi wanaanza kujinyonga wao wenyewe kwa fikra hasi walizokuwa nazo.
Utakapoanza kujiuliza na kutafuta sababu za kwanini huwezi utazipata nyingi sana na mwisho wa siku utaahirisha kile ulichokuwa unataka kukifanya.

Mbaya zaidi kwenye jamii zetu mtazamo hasi ndiyo umetawala hivyo ukiuliza kwanini huwezi ni rahisi kushindwa.

Hatua ya kuchukua leo; acha kutafuta sababu za kwanini huwezi, badala yake tafuta sababu za kwanini unaweza.

Kwahiyo, unaweza kujihamasisha au kutojihamasisha wewe mwenyewe.
Ondoa dhana potofu ya kujiona huwezi na kuwa na mtazamo chanya wa kujiona unaweza.

Kila la heri rafiki yangu,

Rafiki na mwalimu wako,
Mwalimu Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: