Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuepuka Kufanya Maamuzi Ya Kuongozwa Na Hisia

Karibu maamuzi mengi wanayofanya watu duniani yanaongozwa na hisia. Watu wengi hawapendi kufikiri kwani kufikiri ni moja ya kazi ngumu duniani.

Kama ingekuwa tunafikiri kabla tusingekuwa tunafanya maamuzi ya hisia.
Wengi wetu tunaendeshwa na hisia kuliko kuongozwa na akili.

Tunanunua kwa hisia na siyo kwamba kwa uhitaji, bali ule msukumo wa hisia unavyofanya mambo ndani unatupelekea kufanya maamuzi bila kufikiri.

Kufikiri ni moja ya njia sahihi sana ya kutuepusha na mambo mengi yasiyokuwa na maana kwenye maisha yetu.

Kwa kuwa watu wanaongozwa na hisia kama vile hisia za hasira, furaha , upendo, chuki nk, zinapelekea watu kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Kama unafikiri ni sahihi uko sawa, na kama unafikiri siyo sahihi kwako uko sawa pia.

Sasa utawezaje kuepuka kuongozwa na hisia?

Jawabu ni hili;
Jipe muda kidogo wa kufikiria kabla hujachukua hatua.

Ukijiona hujui uchukue hatua gani , umechanganyikiwa, akili ina mambo mengi, tulia pumzika jipe muda wa kufikiria.

Unapojipa muda wa kuchukua hatua, unakuwa unaziondoa hisia ziondoke, na unapata muda wa kufikiria.

Unapojiona hauko sawa, una hasira, unahitaji kujipa muda.
Hata pale unapohitaji kufanya maamuzi sahihi unahitaji upate muda, ikiwezekana lala, pumzika au tembea na ukiamka akili inakuwa imetulia na ni rahisi kwako kufanya maamuzi.

Hatua ya kuchukua leo; Jipe muda , jicheleweshe makusudi kuchukua hatua hatua wakati unapojikuta uko kwenye hisia yoyote ile .

Kwahiyo, huwa tunaharibu sana mahusiano yetu na wengine kwa sababu ya kukubali kuongozwa na hisia.
Tukiweza kutawala hisia zetu na kukubali kuongozwa na akili tutaweza kupunguza matatizo mengi.
Nakusihi anza sasa na utaona matokeo mazuri.

Kila la heri rafiki yangu,

Rafiki na mwalimu wako katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa.
Mwalimu Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: