Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kumwamasisha Mtoto Wako Ili Aweze Kufaulu Sana Darasani

Rafiki yangu mpendwa,

Sisi binadamu huwa tuna vitu viwili ambavyo vinatuhamasisha kuchukua hatua, kitu cha kwanza ambacho kinatuhamasisha kuchukua haraka ni kwa ya kupata furaha au raha na kingine kinachotuhamaisha kuchukua hatua ni kuepuka maumivu.

Ziko hamasa za aina mbili zinazofanya kazi vizuri ambazo ukizitumia utaweza kumwamasisha mtoto wako na kufanya vizuri shuleni. Kila mzazi anapenda kuona matokeo mazuri kwa mtoto wake hivyo matokeo mazuri nayo hayaji hivi hivi yanahitaji kazi ya ziada.

Wazazi wengi huwa wanatumia njia ya adhabu kama ya kumwamasisha mtoto ili kufanya vizuri, kwa mfano, mzazi anamwambia mtoto wake endapo utakapofanya vibaya utapata adhabu fulani. Sasa njia ya adhabu huwa haimwamasishi sana mtoto kuchukua hatua ukilinganisha na hamasa ya zawadi.

Adhabu inamfanya mtoto akose hamasa na kukata tamaa mapema hivyo njia hii siyo afya sana ya kumwamasisha mtoto kama unataka afanye vizuri kwenye masomo.

Njia nzuri ya kumwamasisha mtoto ni kumpa zawadi. Njia ya zawadi inafanya kazi kuliko njia ya adhabu. Ukimwambia mtoto kuwa ukifanya vizuri nitakupa zawadi ya kitu fulani atajituma sana kuhakikisha anakipata kile anachokitaka kwenye masomo yake.

Hata wewe mwenyewe, ukiambiwa zawadi na adhabu ipi utahamasika kuchukua hatua haraka? Nafikiri ni zawadi, kila mtu anapenda vitu vizuri hivyo ukitaka kumkamata mtu ili afanye vizuri tumia mbinu hii ya zawadi.

SOMA; Hii Ndiyo Lugha Bora Ya Kufundishia Watoto

Siyo kwa mtoto tu bali hata kama una watu umewaajiri weka mfumo wa kutoa zawadi pale mtu anapokuwa amefanya vizuri utaona watu watakavyokuchukua hatua na kufanya vizuri kwenye yale wanayotakiwa kufanya.

Hatua ya kuchukua leo; badala ya kumwamasisha mtoto kwa njia ya adhabu kuanzia sasa jaribu mbinu ya zawadi utaona matokeo mazuri.

Kwahiyo, wazazi wengine wanapomuona mtoto hafanyi vizuri wanamwita majina ya ajabu kama vile mjinga huna akili na mengine yanayofanana na hayo. Nakusihi usifanye hivyo hata kama hafanyi vizuri wewe mtie moyo na mwite majina mazuri ya kumwamasisha kuwa sehemu ya faraja kwake na siyo kuwa mwiba wa kumuumiza.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

www.mtaalamu.net/kessydeo

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: