Rafiki,
Ni kawaida katika jamii yetu watu kuona kama vile kazi ni mateso sana.
Watu kufanya au kutimjza wajibu wao wanahisi kama vile ni utumwa na siyo sehemu ya maisha yao.
Tukianzia katika kuamka mapema , mtu akiwa bize na kazi zake wako watakaosema fulani anateswa au anajitesa na kazi.
Hapa tunajifunza kuwa licha ya kuwa kazi ni muhimu sana tena ni rafiki yetu kwa sababu kazi inatusaidia kupata kile tunachotaka katika maisha yetu.
Lakini kuna watu hawapendi kazi, wanahisi kazi ni kama utumwa.
Kazi siyo utumwa bali kazi ni asili ya binadamu tangu kale.
Kitu ambacho hakijawahi kumuangusha mtu katika kazi ni juhudi.
Watu wenye bidii kwenye jambo lolote lile hufanikiwa sana katika kile wanachofanya.
Kama unataka kufanikiwa weka bidii na juhudi utapata matokeo mazuri.
Watu wanajituma sana katika kazi zao na huwa juhudi inamlipa mtu kadiri anavyojitoa.
Jitume utafanikiwa, jali kazi, jali kile ambacho kinakuingizia fedha haya mengine achana nayo.
Uwe rafiki wa kazi, acha kuwa mtumwa wa mambo yasiyochangia faida chanya kwenye maisha yako.
Kama ukiweka juhudi katika kazi, juhudi itakuzawadia matokeo mazuri na wala haijawahi kumuangusha mtu.
Hatua ya kuchukua leo; Juhudi katika jambo lolote ndiyo msingi wa mafanikio.
Kwahiyo, kama unataka kufanikiwa katika jambo lolote lile , nakusihi weka juhudi na utakua na mafanikio mazuri sana kwenye kile unachofanya.
Kila la heri rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Mwalimu Deogratius Kessy
http://www.mtaalamu.net/kessydeo