Mpendwa rafiki yangu,
Wote tunajua kazi ni muhimu sana katika maisha yetu, licha tu ya kuwa muhimu bali imekuwa ni asili ya kila binadamu, binadamu ni kazi huwezi kuendelea kuishi bila kuwa na kazi.
Licha ya kuwa kazi inachosha lakini huna namna inabidi ufanye kazi ili uishi, sasa chagua kufanya kazi, huwezi kufa kwa ajili ya kazi bali utaimarika kwa ajili ya kazi.
Tumekuwa ni watu wa zuri sana wa kuweka mipango, yaani kama ni utajiri basi kila mtu ni tajiri wa kuweka mipango hapa duniani. Kila mtu ni tajiri wa kuweka mipango lakini upande wa pili ni shida.
Kazi ambayo inawashinda watu wengi ni kutekeleza mipango waliyoweka. Mwanzoni mwa mwaka watu wengi wanapanga malengo lakini baada ya muda rudi kuwauliza wamefikia wapi malengo yao watabaki wanakupa sababu nzuri za kwanini walishindwa kutekeleza.
Tumekuwa ni watu wa kujitetea sana pale tunaposhindwa kutekeleza majukumu yetu vizuri, usikubali kupoteza muda wako kwenye kupanga halafu ukashindwa kutekeleza, kile unachopanga basi jaribu kukaa chini na kukifanyia kazi.
SOMA; Jinsi Ya Kuwasha Moto Wa Hamasa Ndani Yako
Hakuna ambaye ameweza kufanikiwa kwa kuweka mipango peke yake bali watu wengi wanafanikiwa duniani kwa kuweka mipango na kuifanyia kazi mipango yao.
Acha kuahirisha mambo, kupanga na kutotekeleza ni njia ya kujidharau mwenyewe, unatakiwa kujikamata mwenyewe pale unapoona hujafanya kile ulichopanga jikamate haraka sana na kifanye ulichopanga kufanya.
Usijionee huruma katika kazi ulizopanga kufanya jisimamie na kuwa na nidhamu bora ambayo itakupa matunda mazuri sana. usiwe katika nafasi ya wapangaji, mpangaji ni sawa na yule mchezaji mpira anayepambana kutoka na mpira golini mwake mpaka kwa mpinzani halafu anafika pale anashindwa kufunga goli na nafasi akiwa nayo.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa sehemu ya kupata matokeo kwa kutekeleza kwa vitendo mipango unayopanga. Unapopanga kumbuka kutekeleza mara moja na kama huwezi kutekeleza basi usipange.
Hivyo basi, mtu makini ni yule anayepanga na kutekeleza kile alichopanga, unapata heshima sana pale unapokuwa mtu wa kupanga na kutekeleza kwenye maisha yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana