Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hizi Ndiyo Hisia Mbili Zinazowasukuma Watu Kuchukua Hatua

Mpendwa rafiki yangu,

Kila mmoja wetu kuna hisia mbili ambazo zinamsukuma mtu juu ya jambo fulani. Watu wa mauzo na masoko ni watu ambao wanatumia saikolojia hii kwa ajili ya kuuza kupitia biashara wanazofanya.

Kila mmoja wetu kuna kitu ambacho anauza hivyo utakapozijua vizuri hisia hizi zitakusaidia katika shughuli zako za kila siku.

Hisia mbili zinazowasukuma watu ni kama vile;

  1. Tamaa ya kupata zaidi; sisi binadamu ni viumbe wa tamaa sana, tunapenda kuwa na vitu vingi katika maisha yetu, asili yetu ni kutokuridhika na ushujaa wetu tunapenda kuuweka katika tamaa ya kumiliki au kuwa na vitu vingi.

Ukiangalia vitu vingi ulivyonunua siyo kwamba ni muhimu sana bali umeongozwa tu na hisia ya tamaa na hatimaye umevipata. Hisia za tamaa zinakusuma sana ni lazima kitu fulani uwe nacho, au ufanye, hivyo tamaa inatumika kama kichocheo kwetu kuchukua hatua fulani.

  1. Hofu ya kupoteza; watu wengi wanasukumwa kuchukua hatua fulani baada ya kusikia kile wanachotaka wanaweza wakakikosa, kwa mfano katika matangazo mengi huwa wanatumia sana hii saikolojia ya kushawishi watu wachukue hatua mara moja na wasipofanya hivyo watakosa nafasi, kama vile kusema nafasi zetu ni chache hivyo wahi mapema kabla hazijaisha.

Hapa inakuwa inamsukuma sana mtu kuchukua hatua, anajijengea akilini kuwa asipochukua hatua sasa anaweza akakipoyeza kile anachotaka. Natumaini umeshawahi kukutana na hili, kwenye makampuni makubwa yanatumia sana mbinu hizi mbili katika mauzo.

SOMA; Vitu Vyote Tunavyovitafuta Tunasukumwa Na Vitu Hivi Viwili

Wanajua kabisa watu wana tamaa ya kupata zaidi, hivyo unahamasishwa kupata zaidi, na kweli unahamasika na kuchukua hatua.

Watu wengi wanaogopa sana kupoteza, hivyo hisia za kupoteza zinawasukuma kuchukua hatua haraka ili waweze kumiliki kitu ambacho wanahisia wakikosa watajisikia vibaya.

Hatua ya kuchukua leo; tumia hisia hizi mbili ulizojifunza hapo juu kwa maendeleo yako binafsi, kuwa makini na hisia hizo hapo mbili. Jua ni wakati gani wa kuzitumia pale unapokuwa unahitaji na kama huna uhitaji hata uwe na hizo hisia siyo lazima kusukumwa kuchukua hatua.

Kwahiyo, ijue kweli, elewa saikolojia ya watu inavyofanya kazi na itumie ili uweze kufanikiwa watu. Tamaa ya kupata zaidi na hofu ya kupoteza ni hisia ambazo zinamwendesha kila binadamu. Kama unataka kuwa vizuri katika mauzo basi tumia hisia hizi mbili kuwasukuma watu kuchukua hatua ili wanunue kile unachouza.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe Na Siku Bora Sana Rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

www.mtaalamu.net/kessydeo

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: