Design a site like this with WordPress.com
Get started

Vitu Vitatu Ambavyo Hupaswi Kuviamini  Kwenye Maisha Yako

Imani tuliyonayo ndiyo inatufanya tuwe hivi tulivyo leo. Maisha ni imani na kila mtu anaongoza maisha yake kadiri ya imani yake.  Unafanya hicho unachofanya leo kwa sababu una imani nacho na kama ungekuwa huna imani nacho usingeweza  kukikifanya.

Viko vitu ambavyo hatupaswi kuviamini kwa asilimia mia moja katika maisha yetu. Muda mwingine tunaweka maisha yetu kwenye matumaini hayo tunajikuta tunaanguka vibaya sana.

Mambo matatu ambayo hatupaswi kuyaamini kwenye maisha yetu ni kama yafuatayo;

Kuiamini kesho; kitu ambacho unatakiwa kukielewa katika maisha yako hakuna kesho. Ukipanga kufanya jamb oleo lifanye leo hakuna mtu anayejua kesho itakuwaje. Kesho huwa inakuja na mambo ambayo hatukuyatarajia. Usiwe na uhakika kabisa na kesho, siku na muda ambao una uhakika nao sasa. Kwenye kila kitu unachotaka kufanya usifikiria muda mwingine bali sasa.

Kesho imewafanya watu wengi kuwa masikini, kuharibu kazi, kuharibu mahusiano. Huwa tunapoteza bahati nyingi sana kwenye maisha yetu kwa kuitegemea kesho. Na huwa tunaahirisha mambo yote haya kwa sababu ya uvivu. Siyo kwamba hatuwezi kufanya sasa ila uvivu unawafanya watu kupeleka mambo mbele.

Kuiamini baadaye; ni mara ngapi huwa tunajiambia baadaye nitafanya moja, mbili , tatu? Lakini inavyokuja hiyo baadaye je tunaweza kuyafanya hapo mambo ambayo tuliamua kuahirisha? Kama mtu uko makini na maisha yako kile ambacho umepanga kufanya fanya kifanye tu. Hata mtu akija kwako na kukuambia hadithi za baadaye au za kesho usimsikilize.

SOMA; Muhimu; Kabla ya Kuanza Wiki Ya Kesho Unahitaji Kuwa Kitu Hiki Ili uweze Kufanikisha Mambo Yako

Ukishakuwa makini na maisha yako, kama hutaki mambo ya kesho au ya baadaye hata wale wanaokuzunguka wanajaribu kuendanana na wewe. Hata mafundi wengi wanapenda sana baadaye na kesho. Wakikuambia hivyo waambie mimi ni mtu wa sasa, sihitaji baadaye wala kesho yako kama unaweza kufanya sasa mwambie akufanyie.

Kuamini ahadi; hapa kuna changamoto kubwa sana. watu wengi wamedanganya na ahadi na imewasababishia hasara kubwa kwenye maisha yao. Kamwe usiwe mtu wa kuiamini au kutegemea ahadi. Ahadi nyingi  watu wengi huwa wanaziahidi kwa hisia sasa inapokuja uhalisia wa kutekeleza ahadi walizoahidi hapo ndiyo matatizo yanapoanzia.

Unaweza kuahidi fedha kwa hisia lakini pale unapokuja kutoa inauma sana. Siku zote anachoahidi mtu kione kama vile upepo umepita lakini usikae na kukiamini kuwa ahadi zitakuja kubadilisha maisha yako. usikae kutegemea ahadi ya mzazi, rafiki, serikali, amka na jitegemee wewe mwenyewe kama mkurugenzi wa maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; usitegemee kesho, ahadi na baadaye. Kila kitu unachofanya kiangalie sasa, kile ambacho kina uhakikaa na siyo vitu ambavyo havina uhalisia.

Kwahiyo, maisha ni yako na amua leo kuishi kwa uhalisia na siyo kuishi kwa kutegemea kesho, ahadi na baadaye. Ukivitegemea vitu hivi tegemea kuanguka tu.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: