Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kulinda Nguvu Zako Na Kuwa Na Uzalishaji Bora

Mpendwa rafiki,

Katika zama hizi watu wengi wamevurugwa na mitandao ya kijamii, mwandishi mmoja anasema watu wamekuwa ni kama misukule wa mitandao ya kijamii. Tafiti zinaonesha kuwa kila baada ya dakika kumi au tano mtu lazima ashike simu yake. Kwa namna kama hii unaona ni jinsi gani nguvu zetu zinakwenda sehemu ambayo siyo sahihi.

Unakuta mtu anaianza siku yake kwa kusoma mitandao ya kijamii, anaanza kusoma kila jumbe aliyotumiwa na kujibu, apitie kila mtandao ajue nini kinaendelea na baada ya muda anajikuta amechoka na hakuna kikubwa alichofanya.

Badala kutumia muda wa asubuhi kujitumikia, yaani kuzalisha kufanya kitu cha maana ambacho kitakusaidia kila siku kwenye maisha yako wewe unaanza siku na kusikiliza habari za watu ambazo hata hazitakuja kukusaidia kwenye maisha yako.

Kama unataka kulinda nguvu zako na kuzitumia nguvu hizo kwenye uzalishaji basi epuka kutawanya nguvu zako. Kuanzia unapoamka anza siku yako kwa kufanya kitu chanya, usikimbilie kuchungulia nini kinaendelea kwenye mitandao yako ya kijamii badala yake weka fokasi katika zako. Hakikisha unatuliza akili kwenye kazi na siyo kwenye simu.

Huwezi kupata uzalishaji mzuri kama kila siku kila siku unafanya kazi huku ukiwa na simu mara unajibu jumbe, hujamaliza huku tena yule mtu aliyekutumia ameshajibu hivyo unakuta unatawanya nguvu kwenye mambo ambayo hayana uzalishaji.

SOMA; Kama Uko Kwenye Maisha Ya Ndoa, Kazi Yoyote Ile Epuka Kabisa Kufanya Kitu Hiki

Usikubali kutawanya nguvu kwenye mambo ambayo siyo ya uzalishaji, weka juhudi kwenye kazi, kazi ndiyo inakufanya upate fedha za kununua vocha na hata hiyo simu yako. Unapofanya huduma yoyote, tafadhali weka simu yako katika hali ya ukimya au zima kabisa. Ni jambo la kushangaza unampigia mtu anapokea simu halafu anakuambia niko kwenye nyumba ya ibada au kwenye kikao kama uko huko unapokeaje simu kama na wewe umeshapoteza umakini wa hapo ulipo.

Pangilia ratiba yako ya kuanzia asubuhi mpaka jioni, tenga muda maalumu ule ambao umechoka ndiyo uingie kwenye mitandao ya kijamii na siyo kila muda unapaswa kuingia kwenye mtandao wa kijamii.

Hatua ya kuchukua leo; linda nguvu zako na usitawanye kwenye mambo ambayo hayana mchango chanya kwako. Tawala uwepo wako kwenye kile unachofanya na acha mengine yapite kwani siyo muhimu kwako.

Kwahiyo, usipokuwa mjanja utajikuta uko bize na mambo ambayo hayana maana na siku inakwisha unajikuta umechoka na huna  kikubwa ulichofanya kwenye kazi.

Makala hii imeandikwa na

Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo, vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: