Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Aina Ya  Upendo Ambao Wazazi Wanapaswa  Kuonesha Kwa Watoto Wao

Ukienda dukani kununua simu, pasi, TV unanunua kile kitu ukiwa umepewa namna ya  kukitumia kile kitu,ndani ya bidhaa utakuta kuna karatasi ya maelekezo.

Hivyo basi, mtoto anapozaliwa hospitali hakuna kitabu cha maelekezo ambacho utapewa namna ya kumlea mtoto. Wengi wanajikuta wanawalea watoto kadiri ya wao walivyolelewa.

Watoto mara nyingi wanapenda kujifunza kutoka kwa wazazi wao kwa vitendo kuliko maelezo. Unapomfanyia mtoto kitu kizuri kwa vitendo anajifunza zaidi. Na unapomfanyia mtoto ubaya wowote ule uwe ni uzalilishaji wa kijinsia, kihisia , kimwili nakadhalika lazima atakuchukia kwa sababu umeacha alama mbaya kwake.

Namna bora ya wazazi wanavyopaswa kuonesha upendo kwa watoto wao ni ule upendo wa vitendo. Kwa mfano, mtoto akiona namna unavyojitoa kuwasaidia wazazi wako, unavyopata muda wa kuwasalimia nao watoto wanakuwa wanajifunza kitu kuwa hata wao wanapokuwa wakubwa wanatakiwa kuwajali wazazi wao kama vile baba na mama wanavyowajali wazazi wao.

Upendo wa vitendo ndiyo upendo uliyo hai. Kila mtu ambaye anaweza kuona anaweza kujifunza. Tunapokuwa tunajali wengine na kuwatendea mazuri hata watoto wanaona na wao wanajifunza kitu kizuri kutoka kwetu.

Mt. Agustino aliwahi kusema, kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Hivyo wewe kama mzazi au mtoto unatakiwa kumpenda mzazi wako bila vipimo vyovyote. Usiangalie mzazi wako vile alivyo bali wewe mtendee mazuri kwa sababu inakupasa kufanya hivyo.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Kuondoa katika Akili Ya Watoto

Kuna changamoto nyingine za wazazi kuwaharibu watoto wao, badala ya kuwafundisha mazuri wao wanawafundisha watoto mambo mabaya.  Kwa mfano, wazazi wa mtoto mmoja mwenye miaka mitano wanafanya kazi ya kuuza pombe eneo fulani, hivyo wale wazazi mara nyingi wanarudi wakiwa wamelewa. Sasa mara nyingi mama ndiyo huwa anauza na baba huwa anamwacha mama kule kilabuni na baba anatangulia kurudi nyumbani.

Siku moja jirani alimuona yule mtoto wa miaka mitano anatembea vibaya, pili ananuka harufu mbaya yule jirani akamfuata na ikabidi amfunue ajue nini kinanuka. Kumuangalia ndani mtoto hafai, amefanyiwa ukatili wa kijinsia na baba yake. Kumbe baba yake anavyowahi kurudi alikuwa ana tabia ya kumwingilia mtoto kimapenzi tena mtoto wa miaka mitano.

Yule jirani ikabidi akatoe taarifa polisi, na kumpeleka mtoto hospitali. Na ushauri wa daktari, alisema yule mtoto inapaswa atolewe kizazi kwa sababu ameharibika sana.

Je kupitia tukio hilo, je yule mtoto ataweza kumpenda mzazi wake kwa kile alichomfanyia? Kumsababishia  hali ya kutokuja kupata mtoto maisha yake yote.

Kama mzazi unatakiwa usiwe na malezi yenye makwazo kwa mtoto wako. Usimfanyie vitu ambavyo havistahili kufanyiwa. Mzazi ndiyo unayepaswa kumpa mtoto ulinzi lakini wazazi wengine ndiyo wanakuwa wa kwanza kuharibu usalama wa watoto.

Hatua ya kuchukua leo; mpe mtoto malezi bora, mlee kwa upendo wa vitendo. Usimkwaze mtoto kwa sababu zako binafsi.

Kwahiyo, kila mmoja anawajibika kuwa mlinzi wa watoto katika jamii yake, mtoto awe ni wako au siyo wako unatakiwa kumlinda katika hatari zote. Usishiriki kumharibu mtoto kwa namna yoyote ile bali kumlinda.  Watoto wanapokuwa wanapitia magumu, wanafikia mahali wanajuta kwanini  hata wamezaliwa kwani dunia imekuwa siyo sehemu salama kuishi kwao.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: