Rafiki,
Tunaalikwa kushukuru kwa kila jambo, lakini siyo kila jambo tunapaswa tu kushukuru nitakuambia baadaye kivipi. Kushukuru ni utamaduni wa kila mwanadamu, tukikosa kushukuru basi tutakuwa hatuna fadhila. Tunaposhukuru ndiyo tunatengeneza nafasi ya kupata zaidi.
Kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako halafu umeshindwa kukifanya hupaswi kukaa chini na kusema nashukuru kwa kila jambo.
Unashindwa kutimiza majukumu yako vizuri, labda ni kwa sababu ya uzembe au uvivu halafu unashukuru hiyo itakuwa sawa? Vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako hupaswi kutumia msemo huu tunapaswa kushukuru kwa kila jambo wakati una uwezo wa kukibadilisha.

Kwa mfano, mtu yuko kwenye madeni na kipato chake ni kidogo badala aweke juhudi kutoka kwenye madeni na kuongeza kipato yeye anafurahia na kusema tunapaswa kushukuru kwa kila jambo.
Yapo mambo ambayo unapaswa kushukuru pale yanapotokea, kwa mfano, mambo ambayo yako nje ya uwezo wako unapaswa kulipokea na kulishukuru kadiri ya lilivyo kuja. Huwezi kubadilisha kwa sababu tayari imeshakuwa ni asili.
Usikubali kushukuru kwa kupokea matokeo ya hovyo kwa sababu tunaalikwa kushukuru kwa kila jambo. Mtu anakufanyia kitu ambacho hukipendi badala ya kuchukua hatua unalalamika na kusema tunapaswa tu kushukuru kawa kila jambo. Siyo kila jambo tunapaswa kushukuru, unatakiwa kuwajibika katika nafasi yako na siyo kukimbilia kujificha kwenye msemo wa kushukuru kwa kila jambo.
SOMA; Mambo Matatu (03) Yakufanya Pale Unapojikuta Njia Panda Hujui Nini Cha Kufanya.
Kama jambo lipo ndani ya uwezo wako unaweza kulibadilisha hupaswi kusema unashukuru kwa kila jambo badala yake unatakiwa kukomaa mpaka uone matokeo. Kuna vitu vingine viko ndani kabisa ya uwezo wetu ila tunakuwa wagumu kukubali kupokea matokeo kama yalivyo bila kuhoji ukweli.
Kwenye kazi yako hupati kipato kikubwa badala yake unaishia kulalamika badala ya kuchukua hatua ya kuongeza thamani ili kipato kiongezeke, wewe unashukuru tu. Hupaswi kukaa chini na kusema nashukuru kwa kila jambo hata hilo la kipato kidogo. Kuwa na kipato kikubwa au kidogo ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako unao uwezo wa kubadilisha matokeo na kuwa vile unavyotaka wewe.
Kwenye biashara unayofanya kama unaona mambo hayaendi vizuri usiridhike kwa kusema unashukuru kwa kila jambo hapana, kaa chini angalia nini tatizo, kama hutoi huduma bora anza sasa kutoa thamani kubwa na wateja watakuja kwa wingi.
Kwenye malezi ya watoto huwezi kusimama na kusema jamani hawa watoto mimi wamenishinda sasa kama watoto ni wako wamekushinda unafikiri nani atawaweza? Usikimbie matatizo yako bali ya kabili kwa kuona ukweli.
Kwenye mahusiano ya ndoa labda mwenza wako siyo mwaminifu halafu unaridhika kwa kusema nipaswa kushukuru kwa kila jambo, chukua hatua ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako kama mkikaa chini na kueleweshana lakini kwa kuongea tu bila kuchukua hatua ni sawa na bure.
Hatua ya kuchukua leo; kama kitu kipo ndani ya uwezo wako usikubali kuridhika na matokeo uliyopata au unayopata badili haraka sana kwa kipo ndani ya uwezo wako. Huna muda wa kusema unashukuru kwa kila jambo wakati jambo lenyewe lipo ndani ya uwezo wako.
SOMAM; Haya Ndiyo Mahusiano Magumu Katika Zama Hizi Za Taarifa
Kwahiyo, tusikimbilie kujificha kwenye sababu za kushukuru vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu. kama kitu kipo nje ya uwezo wako na huwezi kukibadili sawa lakini kama unaweza kukibadili hupaswi kushukuru. Kwa mfano, kutokunyesha kwa mvua ni jambo ambalo liko nje ya uwezo wako hapo huna ujanja, unaweza tu kushukuru kwa kile kilichotokea.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy