Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kipimo Cha Kuonesha Kama Umeelewa Kitu

Mara nyingi unapokuwa unafundisha unatakiwa kuwaelezea wanafunzi kwa lugha rahisi ili waweze kukuelewa. Kumfundisha mtu kwa lugha ngumu ambayo haielewei huo ni ujinga.

Aliyekuwa mwanafizikia Einstein aliwahi kusema, kama huwezi kuelezea kitu kwa lugha rahisi basi hujakielewa.

Kwahiyo, kipimo cha kuonesha kama wewe umeelewa kitu ni kuwaelezea wengine kwa lugha rahisi. Ukiona huwezi kuelezea kwa lugha rahisi jua kabisa hujakielewa kitu hiko.

Kama unataka kuelewa kitu basi kisome na kielewe vizuri halafu tumia lugha rahisi kuwaelezea wengine. watu wengine wanaamini kuwa ukitumia lugha ngumu ndiyo utaonekana unajua kumbe huo ni ujinga.

Plato yeye aliwahi kusema, mwerevu huongea kwa sababu ana kitu cha kusema na mjinga huongea kwa sababu inabidi aseme kitu. usiwe kama mjinga kuwa mwerevu kama kitu hujakielewa na umeshindwa kukielezea kwa lugha rahisi hii ni alama ya wazi sana hujakielewa kitu hiko.

SOMA; Jinsi Ya Kufanya Kazi Yoyote Kuwa Rahisi

Kwa wale ambao wanatumia muda wao kuwafundisha wengine, hakikisha kwanza kile unachofundisha wewe unakielewa, na kama unakielewa unaweza kukielezea kwa lugha rahisi. Ukishindwa kuelezea kwa lugha rahisi hii ina maana kwamba wewe mwenyewe hujakielewa.

Sasa kama kitu hujakielewa utawezaje kwenda kuwafundisha watu wengine waweze kuelewa?

Hatua ya kuchukua leo; kama huwezi kuelezea kitu kwa lugha rahisi basi hujakielewa kitu hiko hivyo basi elewa kwanza ndiyo ukawaelezee watu kwa lugha rahisi.

Rafiki, usifanye mambo kuwa magumu bali fanya mambo kuwa marahisi. Ukitaka kuwasaidia watu kitu jitahidi kukirahisisha zaidi. Usiwafundishe watu au kuwasaidia kwa katika hali ngumu kama unaweza kufanya kwa kurahisha fanya hivyo ili uwasaidie wengine kuelewa kwa urahisi na huo ni ujanja lakini ujinga ni kutumia lugha ngumu au kufanya mambo kuwa magumu kwa wengine ili wakuogope.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: