Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukienda Sokoni Nunua Mahitaji Usinunue Maradhi

Ukienda sokoni jitahidi sana kununua mahitaji muhimu sana na siyo maradhi. Wengi huwa tunaenda sokoni lakini hatuendi kununua mahitaji bali tunaenda na mengi ambayo yanatusababishia kuyapata ambayo siyo muhimu.

Ukiwa na fedha mkononi unatakiwa kuwa makini sana, maana fedha uliyonayo inaweza kukusaidia kununua maradhi au uhai.

‘’ nimewapeni uchaguzi kati ya uhai na kifo, kati ya Baraka na laana. Basi chagueni uhai nyinyi na wazawa wenu mpate kuishi’’

Unapopata fedha jitahidi sana kununua uhai na siyo maradhi kwani tunatumia pesa tunayoipata kujiharibu sisi wenyewe.

Ukienda sokoni nunua mahitaji muhimu yatakayoweza kulinda uhai wako. Wako wanaonua magonjwa wakienda sokoni na wako wanaonunua mahitaji muhimu wakienda sokoni.

Sisi ndiyo watu wenye dhamana ya kulinda uhai wetu au kuupoteza. Tunaalikwa kuwa makini sana na yale tunayofanya. Kila siku hakikisha unanunua kitu ambacho kitalinda uhai wako na siyo kuupoteza.

Ukianzia kwenye chakula nunua vyakula vitakavyolinda mwili wako na siyo vitakavyoharibu mwili wako. Anayefanya afya yako iwe nzuri au mbaya  ni wewe mwenyewe. unajinunulia vitu ambavyo havilindi wala kuupa mwili kinga dhidi ya magonjwa.

SOMA; Fursa Tatu Za Kipekee Zitakazokuwezesha Kukua Kiakili Na Kutanua Wigo Wa Maarifa

Kwenye akili, nunua vitabu na maarifa mbalimbali yatakayoweza kuipa akili yako uhai. Usikubali kuipa maradhi akili yako kwa kuingiza maarifa yasiyofaa kwenye akili yako. Mtu akija na kuanza kuchezea mwili wako bila ridhaa yako utakuwa mkali sana lakini akichezea akili yako wala huna hata shida. Unachezewa akili yako na mitandao ya kijamii kwa kusoma kila habari inayokuja mbele yako.

Uwe mtu wa kununua uhai kwenye kila eneo la maisha yako na siyo maradhi. Maradhi yataondoa uhai wako mapema lakini uhai unalinda uhai wako.

Hatua ya kuchukua leo; ukishika fedha, nenda kanunue uhai na siyo maradhi. Unapokuwa una fedha unanunua uhai au maradhi.

Hivyo basi, tumia akili yako kutumia fedha uliyonayo vizuri kununua vitu vitakavyokupa uhai na siyo maradhi. Usikubali kujiua mwenyewe kwa kununua vitu ambavyo vinachangia kuharibu uhai wako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: