Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Usipoteze Siku Yako Fanya Kitu Hiki

Rafiki,

Kwa zama hizi za taarifa watu wamekuwa ni mabingwa wa kupoteza siku zao. Watu wako bize lakini hakuna kikubwa wanachoingiza wazungu wanasema busy for nothing. Changamoto ya zama hizi ni kwamba mitandao ya kijamii inawachangia sana kuwavuta watu kuvunja siku zao.

Siku moja nilikuwa na mwadhiri wa chuo kikuu fulani, akaniambia yaani nikiamka nikishika simu yangu, nikishapitia tu kidogo nakuja kushtuka tayari muda umeenda na sijafanya la maana. Ndivyo ilivyo kwa watu wengi.

Watu wengi wanaanza siku zao bila kupangilia nini wanakwenda kufanya. Hawajui kupangilia muda wao yaani wao wanakuwa wanaongozwa na matukio yanayoendelea kutokea. Wanasema kama umeanza siku yako na hujui nini unakwenda kufanya rudi kitandani ukalale.

Kama unataka usipoteze siku yako basi wahi kuamka alfajiri, anza kuamka kuanzia saa 10 mpaka saa 11. Ukichelewa kuamka ni mwanzo wa kupoteza siku yako, kwanza utaanza kukimbizana na muda utafanya vitu haraka haraka kwa kutaharuki. Na mtu anayekuwa anakimbizana na muda huwa anakuwa anashindwa kuleta ufanisi.

Amka mapema, usikubali usingizi ukutawale. Kuwa na kiwango cha muda  wa kulala na wa kuamka ukifika kiache kitanda. Ukiwa ni mtu wa kusikiliza mwili wako huwezi kufanikiwa hata siku moja. Miili yetu inapenda sana kusikilizwa, ukiipa demokrasia kila siku itakuwa inashinda.

Unatakiwa kusema hapana kwa mambo ambayo hayana mchango chanya kwako. Kusema hapana ni mwanzo mzuri wa kuanza nidhamu binafsi, ukiwa ni mtu wa ndiyo utakuwa ni mtu wa kupoteza kila siku. Siyo kila kitu ni cha kuruhusu kiingie kwenye maisha yako, kuwa mbinafsi wa muda wako kabla vile unavyokuwa makini kwenye fedha.

SOMA; Jinsi Ya kuuwahi Muda Kabla Haujakuwahi Wewe

Amka asubuhi na mapema nenda kafanye kazi kama binadamu. Hujui ya kwamba kufanya kazi ni asili ya binadamu? Kiache kitanda na nenda kawajibike ili uweze kupata kile unachokitaka. Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kuendekeza usingizi.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka usipoteze siku yako wahi kuamka mapema. Ukiwahi kuamka utaweza kuipangilia siku yako na hatimaye kuinza siku ukiwa unajua nini unakwenda kufanya.

Kwahiyo, kama hujui nini unataka basi huwezi kupata kile unachotaka. Maisha ni kujitoa kwenye kile unachotaka mpaka uhakikishe umekipata kweli. Usijionee huruma kama kweli unataka kuona mabadiliko chanya.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: