Rafiki,
Huwa ni kawaida ya binadamu kukutana na changamoto, kama unaishi basi huwezi kulikwepa hilo kwenye maisha yako.
Huwa tunapopatwa na matatizo muda mwingine tunayatatua matatizo hayo kwa njia ya hisia na siyo kwa kutumia akili. Na kitu kinachotatuliwa kwa hisia huwa kinakuja kuwa na athari baadaye, tukiwa ni watu wa kutatua au kufanya maamuzi kwa njia ya hisia tutakua tunapotea njia kila siku.
Waandishi wa kitabu cha Stealing Fire wanasema, matatizo magumu yanapotatuliwa kwa njia rahisi yamekuwa yanatengeneza matatizo zaidi.
Kumbe basi, tukiwa ni watu tunaotatua matatizo kwa njia rahisi lazima tutengeneze matatizo zaidi ndani yetu.
Hivyo basi, kabla ya kukimbilia kutatua tatizo, kaa chini kwanza fikiria namna bora ya kutatua tatizo. Huwa tunakimbilia kutatua lakini hatukai chini kufikiria njia bora ya kutatua tatizo ndiyo maana muda mwingine matatizo yanayojitokeza mara kwa mara ni kwa sababu mwanzo kutopata majibu ya uhakika.
Unapopatwa na tatizo lolote lile, kaa chini fikiria ni njia gani unaweza kutatua tatizo ambalo unalo. Usikimbilie tu kumaliza kwa njia ambayo siyo bora ya kutatua tatizo.
SOMA; Hiki Ndiyo Chanzo Cha Matatizo Mengi
Mara nyingi tunapojua kiini cha kosa tunakuwa huru kutatua tatizo tulilokuwa nalo. Kama unatatua tatizo, hujajua kiini cha tatizo halafu huna namna bora ya kutatua tatizo unakuwa katika hali ngumu sana, badala ya kutatua tatizo utakua unaongeza tatizo zaidi.
Hatua ya kuchukua leo; kabla ya kutatua tatizo, kaa chini fikiria namna bora ya kutatua tatizo.
Kwahiyo, kwenye maisha tunapotatua tatizo moja siyo kumaliza matatizo. Tunapaswa kulijua hilo, unapotatua tatizo moja jua kuna mengine mbele yatafuata. Ni vema kujiandaa na kukabiliana na matatizo muda wowote na kufikiria njia bora ya kutatua tatizo.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.