Mpendwa rafiki,
Kila mmoja wetu anakosea, na anafanya makosa pia. Hakuna binadamu aliyekamilika na ambaye hafanyi makosa. Watoto wadogo wanapojifunza katika shule za awali huwa wanatumia penseli na ufutio kwa sababu wanapojifunza huwa wanakosea sana, wanapokosea wanafuta na ndiyo maana hawatumii kalamu kujifunza.
Jiamini kuwa wewe ni mtu bora katika ufanyaji wa kitu fulani, ila kujiamini kwako kusikufanye ujisahau na kushindwa kujikagua vizuri kwa makosa madogo.
Ndiyo maana tuko wengi hapa duniani, ukiwa na kazi yako wape watu wengine waipitie kwanza kabla hujaitoa kwa watu waione. Kuna mchakato mkubwa mpaka pale unapoiona kazi ya mtu fulani iko bora, hii huenda ni kwa sababu ya umakini wa kuhakiki.
Chochote unachofanya jiamini lakini thibitisha kile unachokiamini. Kama umefanya kazi fulani kabla ya kuiwasilisha hebu kaa chini uikague kwanza hiyo kazi ndiyo uiwasilishe.
Usikubali kuamini bila kuthibitisha, taarifa yoyote unayopewa ithibitishe kwanza. Kwa mfano, msaidizi wako wa kazi akikuambia amefanya kitu fulani amini lakini nenda kathibitishe, hakikisha kwanza kama amekifanya kweli.
Tutakapokuwa watu wa kuthibitisha tunawajengea umakini hata wale tunaofanya nao kazi kuwa sisi siyo wa kawaida, ni watu makini ambao tunafuatilia kila hatu tunachoambiwa.
SOMA; Jinsi Ya Kujifunza Kuwa Mtu Makini Katika Maisha Yako
Kwa njia hii ya kuamini na kuthibitisha utaweza kupunguza uzembe mwingi unaotokea. Kwani watu wengi wanafanya makosa mengi kwa sababu ya uzembe. Tunaweza kuzuia uzembe kwa kuwa makini, kuthibitisha na kukagua kila tunachoambiwa.
Usiwe mtu wa kuamini tu bila kuthibitisha,unaalikwa kuamini lakini thibitisha kwanza kwenye kile ulichoambiwa je ni sahihi? Kujiridhisha ni kitu muhimu sana katika maisha yetu.
Hatua ya kuchukua leo; amini kile unachoambiwa lakini kithibitishe kwanza kabla hujachukua hatua.
Kwahiyo, tunaweza kujenga jamii ya watu makini kama kila mmoja wetu atakua anathibitisha kila kazi anayofanyiwa. Usikubali kwa mdomo bali kubali kwa kuthibitisha kwani, uaminifu umekuwa ni kitu adimu sana miongoni mwa watu wengi.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.