Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Maana Halisi Ya Maadili Hapa Duniani

Watu wamekuwa ni watu wa kushikilia maadili ambayo hayana maana. Tunashikilia maadili hata kama si sahihi kwa sababu ya nidhamu ya uoga. Katika kuendesha dunia kwa usawa tunatakiwa kuangalia kuongozwa na akili kuliko hisia na tuwe huru kubadilisha chochote kile katika maisha yetu pale tunapoona kitu hiki siyo sawa hata ndiyo utaratibu ulioweka.

Watu wenyewe mamlaka fulani wanaweza kuvunja usawa na tukashindwa kumwajibisha kwa kisingizio au kuwa na nidhamu ya uwoga kuwa maadili yetu hayaruhusu kufanya hivyo.  Tumekuwa watumwa na mila na desturi ambazo wameziashisha watu ambao hata hawapo duniani leo lakini watu wanaendelea kuzing’ang’ania.

Kuna maadili ya makabila yetu ambayo yamekuwa vifungo vikubwa sana katika jamii yetu. hebu fikiria katika maadili ya kabila lako hakuna kitu ambacho hukipendi lakini unaendelea tu kukitukuza na kukifuata kwa sababu eti ni maadili ya kabila lako?

Tunatakiwa kurudi nyuma, na kuangalia mbele sasa je haya maadili ambayo yamepitwa na wakati yanatusaidia nini? Ukiona haya kusaidii kitu bali yanakuwakera achana nayo. Chukua kitu amabcho kina msaada na siyo ambacho kina kandamiza wengine. wako watu ambao wanateseka na maadili ya dini,kabila zao wanashindwa kufanya kile ambacho ni sahihi kwa sababu wamefungwa na mila na desturi.

Ni wakati sasa wa kuelewa maana halisi ya maadili, maana halisi ya maadili ni kuelewa na kupunguza mateso kwako na kwa wengine.

Kwa kile unachofanya jiulize kinaleta mateso gani kwako na kwa wengine? ni zoezi rahisi litakaloteta maana ya maadili kwako na kwa wengine.

Ukiona ni maadili ambayo yanaleta mateso kwako na kwa wengine yaepuke mara moja. Fanya kile ambacho hakikuumizi wewe binafsi na wengine.

SOMA; Changamoto Tatu Zinazoikabili Dunia Ya Leo

Kata minyororo ya utumwa ya kushikilia maadili yanayoumiza watu na wewe mwenywe. Ishi kwa kutenda wema, malipo ya wema utayapata hapa hapa duniani hali kadhalika ya ubaya na hii ni kadiri ya sheria ya karma.

 

Hatua ya kuchukua leo; kama maadili unayoishi yanatesa watu na kukutesa wewe mwenyewe achana nayo. Ishi katika maana halisi ya maadili kama nilivyokueleza hapo juu.

Kwahiyo, tutapunguza mateso kwetu wenyewe na hata kwa watu wengine na hapo ndipo tutaifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: