Rafiki,
Watu wengi waliofanikiwa huwa wanakuwa na sifa moja ambayo inafanana. Mtu aliyefanikiwa utamjua tu hata kwa kumwangalia kwa macho.
Mtu aliyefanikiwa huwa hajioneshi bali mafanikio yake mwenyewe ndiyo yanajionesha kuwa yeye ni mtu wa namna gani.
Watu waliofanikiwa wanasifa moja ambayo ni ya unyenyekevu. Watu waliofanikiwa wanakuwa wana unyenyekevu kweli ukilinganisha hata na wale waliofanikiwa. Wanakuwa wanyenyekevu kwa sababu wanajua mafanikio walioyopata waliyatolea jasho na wanajua kuwa watu ndiyo msingi wa vyote tunavyota katika maisha yetu.
Hata ukienda katika ofisi mbalimbali mmiliki au mkubwa wa kazi anakuwa na unyenyekevu na kuhudumia watu vizuri kwa ukarimu ukilinganisha na yule aliyeajiriwa. Watu ambao hawajafanikiwa ni watu ambao wanakuwa hawana unyenyekevu. Wanaongea vile wanavyojisikia na wanakuwa ni watu wenye lawama nyingi sana.
Watu waliofanikiwa hawafanyi maisha kuwa magumu ukilinganisha na watu ambao hawajafanikiwa. Watu ambao hawajafanikiwa ndiyo watu ambao wanakuwa watumiaji wabaya fedha. Wanatumia fedha vibaya ukilinganisha na yule mtu aliyefanikiwa.
Watu waliofanikiwa wanakuwa wanaishi maisha yao bila kukimbizana na watu wengine. wanajali yao sana ndiyo maana wanafanikiwa. Wanakuwa hawaendeshwi na dunia yaani mambo ya nje bali wanakubali kujitawala na mambo yao ya ndani.
SOMA; Sifa Pekee Inayokutoa Katika Kundi La Wanamafanikio
Mtu aliyefanikiwa anakuwa ana nidhamu sana ukilinganisha na watu ambao hawajafanikiwa. Ukitaka kufanikiwa anza kwanza kuwa na nidhamu kwenye kila eneo la maisha yako. jitawale na jiongoze kwenye kila kitu.
Hatua ya kuchukua leo; jijengee tabia bora za kitajiri, angalia tabia bora wanazoishi matajiri na wewe anza kujijengea.
Hivyo basi, maisha huru utayapata mpaka pale utakapojitambua na kuweza kufanya kile unachopaswa kufanya. Huwezi kufanikiwa kama hujui unataka nini kwenye maisha yako0. Jua hakika unataka nini na nenda kakifanyie kazi vile unavyotaka kuwa.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.