Mpendwa rafiki,
Katika uongozi wowote ule unahitaji utu, siyo kwamba wewe ukiwa kiongozi ndiyo unatakiwa kutumia matakwa yako kama vile unavyotaka wewe. Yaani wewe uko juu ya sheria, yaani rule of law.
Tunatakiwa kutumia matakwa yetu vizuri, ili tuwe na uongozi bora ndani yetu tunaalikwa kuwa na kitu hiki;
Unyenyekevu, tunaalikwa kuwa na unyenyekevu katika maisha yetu siyo tu ya uongozi bali hata mengine.
Unyenyekevu katika uongozi unatupatia sifa bora ya uongozi ndani mwetu. Tunapokuwa na unyenyekevu, tunajishusha chini na kwenye uongozi tunatakiwa kukubali sisi kuwa wa mwisho na wengine wawe wa kwanza.
Tunatakiwa kuwaona wenzetu kwanza halafu na sisi tuwe wa mwisho, lakini tunapopenda kujiona sisi mbele na kujitanguliza mbele na kusahau wengine tunakuwa tunatengeneza ubinafsi.
Tukishakuwa na upendeleo au ubinafsi katika uongozi tunatengeneza mpasuko mkubwa kwa wale tunaowaongoza.
SOMA; Huu Ndiyo Uwezo Mkubwa Wa Kila Kiongozi Anaopaswa Kuwa Nao
Hutakiwi kuonesha upendeleo wa wazi wazi katika nafasi yoyote uliyokuwa nayo. Hata kama wewe ni baba au mama katika familia epuka sana kuendesha familia kwa upendeleo utaigawa familia na kusababisha mpasuko mkubwa.
Na ukishazaa chuki katika nafasi yoyote ya uongozi tegemea kuvuna mauti. Chuki huzaa mauti na upendo huzaa upendo.
Tuwatumikie watu kwa unyenyekevu kadiri ya huduma tunazotoa. Tusiwabague bali tuwahudumie kwa upendo.
Hatua ya kuchukua leo; unyenyekevu ndiyo sifa ya kiongozi anayeweza kusikiliza. Usipokuwa na unyenyekevu utashindwa kusikiliza na kuhudumia.
Kwahiyo,kila siku unatakiwa uwe na unyenyekevu na unyenyekevu utakupandisha juu kinyume chake ni kufilisika kiutawala.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.