Rafiki,
Maisha yetu yanaathiri watu wengine kwa kiasi kikubwa sana, kama tutakuwa tunaishi maisha yenye mchango chanya kwa wengine basi tutatukuwa tunawaathiri sana wengine na kufanikiwa kwa vile tunavyofanya na tunavyoishi.
Leo hii nakupa kazi moja rafiki yangu, nenda kajitafakari je wewe unasemwa kwa mazuri au mabaya?
Dunia huwa inatupa kile tunachokitoa nje, usitegemee unatoa chuki halafu ukajiandaa kupokea upendo.
Jitafakari hivi maisha yangu ninasemwa kwa mazuri au mabaya? Hivi majina yetu yakitajwa yanatajwa kwa mazuri au mabaya?
Watu wanapoliona jina au wanaponiona wanafarijika na kujivunia?
Je nina uadilifu ndani yangu wa kuishi maisha yanayompendeza Mungu? au ninaishi tu kuwafurahisha binadamu? Tuishi kuwafurahisha watu, imeandikwa kwamba, amtegemeaye binadamu amelaaniwa.
Usifanye kitu ili watu wakuone, wewe fanya kama ni kazi yako fanya kweli na matunda ya kazi yako yataonekana. Unapofanya kitu fanya kwa moyo na wale watakaopenda kuambatana na wewe watakuja wenyewe.
SOMA; Tafakari Bora Ya Wiki Yenye Mafanikio Makubwa Ya Wiki Inayoanza Kesho
Sisi binadamu ni sumaku, huwa tunavuta wale watu wanaofanana na sisi, angalia karibu marafiki wote ulionao mnafanana kwa vitu vingi.
Ni bora kusemwa kwa yale mambo chanya yenye mchango kwa watu kuliko kusemwa na mambo mabaya ambayo hayana mchango kwa jamii.
Huwezi kufanikiwa kama wewe ni mtu unayesemwa kwa mabaya tu. Utafanikiwaje kama watu unaowatumikia huwatendei haki? Tunatakiwa tuwatendee haki watu kwa sababu mafanikio unayotaka au huduma unayotaka lazima utaitoa kwa watu.
Huduma tunazotoa zinakuwa siyo huduma kama hazina watu wakupokea ile huduma tunayotoa nje.
Hatua ya kuchukua leo; jitafakariĀ je , unasemwa kwa mabaya au mazuri?
Kwahiyo, huenda maisha yako ni kelele kwa watu na siyo sauti. Angalia kama unawapigia watu kelele au unatoa sauti nzuri ambayo kila mmoja akiisikia anafarijika. Je maisha yako ni sauti au kelele.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.