Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiishi Bila Kuwa Na Kitu Hiki Katika Maisha Yako

Sisi binadamu ni viumbe wa hisia na kila binadamu yuko katika mahusiano ni mpango wa Mungu kila bindamu kuwepo katika mahusiano. Una mahusiano ya familia yako, wazazi, ndugu, nakadhalika. Mahusiano ndiyo yanafanya maisha yetu kuwa mazuri au mabaya.

Kama tukiwa na fedha na mahusiano yako vizuri basi maisha yanakuwa mazuri na ya kitajiri, kwani maisha ni mazuri ukiwa na kitu cha kufurahia. Lakini rafiki yangu, maisha yanakuwa magumu sana kama huna fedha na mahusiano hayako vizuri.

Mahusiano yanatuathiri sana, kama mahusiano yetu yako vizuri hata ufanisi wetu maeneo ya kazi unaonekana. Lakini ikitokea mahusiano yako hayako vizuri basi kila kitu kinakwenda vibaya.

Muda mwingine tunakwazana kwenye mahusiano yetu na tusipoombana msamaha basi ni kama  tunaendelea kuweka chumvi kwenye kidonda kibichi. Unatakiwa upalilie mahusiano yako yawe vizuri kuanzia eneo la familia mpaka la kazi. Ukiwa na mahusiano mazuri ya watu utakuwa na matokeo mazuri sana lakini kinyume chake ni hasara.

Usiishi bila kuwa na mahusiano bora na wengine na kila siku unatakiwa kupanga muda wa kujenga mahusiano yako. Tenga muda kila siku wa kuwasiliana na watu wako wa karibu. Angalau kila siku unapata muda wa mawasiliano na mtu mmoja. Kwa kufanya hivi kwa mwaka utakua umeimarisha sana mahusiano yako.

SOMA; insi Ya Kunogesha Mahusiano Yako

Mahusiano ni kitu muhimu sana ambacho kila mmoja wetu hawezi kukwepa kama binadamu. Huwezi kusema sihitaji kuwa kwenye mahusiano wakati hapo ulipo uko na mahusiano na wazazi wako, na ukishakua binadamu basi wewe ni kiumbe wa mahusiano.

Jitahidi kuboresha mahusiano yako, mahusiano mengi hayana afya kabisa, yako katika hali ya hatari. Unapokuwa na mahusiano bora hata mafanikio lazima utakua nayo. Unajisikia faida gani pale unapokuwa na kila kitu halafu mahusiano yako ni mabovu? Familia yako ni mbovu? Huna mtu wa kufurahia naye mafanikio yako?

Hatua ya kuchukua leo,jaza tanki la upendo katika mahusiano yako, toa muda katika mahusiano na kila siku hakikisha unakuwa na ratiba ya kujenga mawasiliano angalau unasalimiana hata na mtu mmoja kwa kumpigia simu au njia nyingine.

Kwahiyo, siyo tu unatakiwa kujenga mahusiano ya kifamilia, kindugu hata mahusiano ya kibiashara au kazi. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako, wapigie  kuwasalimia nao watajisikia na kujiona wanathaminiwa.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: