Rafiki,
Kila mtu anataka kuwa na siku bora, hivyo huwezi kuwa na siku bora kama hujui jinsi ya kuwa na siku bora katika maisha yako.
Ukitaka kuwa na siku bora, tawala kwanza mawazo yako. usikubali uendeshwe na hisia yoyote bali kubali kuingozwa na akili kwanza.
Chochote unachotaka kufanya rudi kwanza kwenye kufikiri kwanza kabla ya kutenda. Fanya maamuzi pale ambapo akili yako imetulia haijataharuki ndiyo utaweza kufanya maamuzi mazuri na siyo vinginevyo.
Ukiendekeza hisia jua kabisa utakua na siku ya hovyo, hisia hazijawahi kumwacha mtu salama. Akili yako ndiyo itawale kila kitu na siyo matamanio ya mwili wako.
Ukitawala akili yako, utakua na siku bora, kwani akili yako ndiyo kama ufunguo wa kufunga na kufungua kile unachotaka kiingie ndani yako.
Usiruhusu akili yako kufikiria vitu ambayo ni hasi, bali ipeleke akili yako kufikiria vitu unavyotaka na utavipata kweli.
SOMA; Mbinu Bora Ya Kukuhakikishia Ushindi Katika Siku Yako Hata Kama Hujisikii Kufanya Chochote Kile
Hatua ya kuchukua leo; ondoa mawazo hasi katika akili yako na uchanya utawale na utakuwa na siku bora .
Kwahiyo, tukishindwa kujitawala tutakuwa tumeshindwa kujiongoza. Mchezo mzima wa mambo yote yako katika akili zetu. Hivyo akili zetu ndiyo chemchem za mafanikio tunayotaka.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.