Rafiki,
Kila kitu katika maisha yetu ni tabia. Tabia tulizonazo leo tulizianzisha sisi wenyewe hivyo katika kila jambo huwa tuna vuna kile tulichopanda.
Matokeo unayopata sasa hivi ni kutokana na kile ulichopanda. Hata katika mambo ya fedha tabia ulizonazo leo ni kutokana na tabia ulizojijengea huko nyuma.
Unachotakiwa sasa ni kuvunja tabia zote hasi ambazo zinakufanya uwe mtumwa katika mambo ya fedha. Fedha inahitaji kujengewa nidhamu ili uweze kuimiliki vizuri, ukiwa na tabia nzuri ya kujijengea nidhamu ya fedha hazitokukimbia.
Fedha zitakufuata kama ukiwa na tabia zinazoendana na fedha. Pia fedha zitakukimbia kama ukiwa na tabia mbaya za kifedha.
Tabia mbaya za kifedha ni kama vile ukipata fedha unatumia kwanza na unakuja kushtuka fedha zimeisha na hujui hata wapi zimekwenda. Ukiwa na fedha unaitumia vibaya bila kujua kuwa itaisha na kesho utahitaji tena.
Huwa utamaduni wa kujilipa wa kujiwekea akiba. Watu wengi wakipata fedha wako tayari kuwalipa watu wengine lakini hawako tayari kujilipa wao wenyewe. Ni kitu cha ajabu sana, mtu yuko radhi kuwanunulia watu wengine lakini hayuko radhi kujiwekea akiba.
Katika mambo ya fedha watu wamekuwa hawana nidhamu ya fedha, wakipata fedha wanawafikiria wengine kwanza badala ya kuanza kujifikiria wao wenyewe kwanza. Kila kitu kinahitaji nidhamu, kama umeshindwa kuitawala fedha lazima fedha itakutawala na kukuendesha.
SOMA; Punguza Matumizi Haya Ya Kifedha Ili Uweze Kufanikiwa Kiuchumi
Hatua ya kuchukua leo; jijengee tabia chanya za kifedha, ambazo ni kujilipa, kuweka akiba na kupunguza matumizi na kuongeza kipato.
Kwahiyo, unatakiwa kuondoa tabia hasi za kifedha ambazo zinakufanya uendelee kudidimia katika mambo ya uchumi. Itumie vizuri fedha unayoipata nayo itakuwa rafiki yako lakini ukiitumia tofauti itakuadhibu tu baadaye.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.