Mpendwa rafiki,
Tulipoanza mwaka kila mmoja wetu aliweza kuweka malengo na mipango mbalimbali lakini, ni watu wachache sana walioweza kwenda na malengo na mipango waliojiwekea. Kupanga ni kazi rahisi ambayo kila mmoja anaiweza kufanya. Lakini utekelezaji ndiyo kazi ngumu ambayo kila mmoja wetu anashindwa kuifanya.
Tumekuwa ni watu tunaojivunia malengo au mipango tuliyonayo kwa wenzetu, kama ingekuwa kuweka mipango ndiyo kufanikiwa basi kila mmoja leo hii angeweza kufanikiwa.
Tunapaswa kuwaonesha watu matokeo yetu na siyo mipango yetu. Matokeo ndiyo habari ya mjini lakini mipango yako baki nayo mwenyewe tu. Watu siku hizi wamekuwa ni mabingwa wa kuonesha mipango au malengo lakini siyo matokeo.
Kuwa bingwa wa kuonesha watu matokeo, matokeo ndiyo mafanikio yenyewe tunayotaka. Hakuna mtu anayehitaji malengo au mipango yako, bali watu wanataka kuona matokeo kwani mipango na malengo kila mtu anaweza kuwa nayo lakini siyo kila mtu anaweza kuwa na matokeo ya mipango au malengoa aliyojiwekea kwenye maisha yake.
Unatakiwa kuwa mtu wa matendo, mtu wa kufanya na washangaze watu kwa matokeo unayofanya na siyo kwa mipango au malengo.
Unapopanga kufanya kitu basi, hakikisha unakitekeleza. Mafanikio yako kwa wale wanaotekeleza na kuonesha matokeo ya kile walichofanya.
Matokeo huwa yanaongea yenyewe, ukifanya kitu watu wanaona umefanya nini hivyo ni wewe kukazana na utekelezaji wa kile ulichoahidi na siyo vinginevyo.
SOMA; Kama umeweka Mipango Na Malengo Yoyote Mwaka Huu Usiache Kusoma Hapa
Huna haja ya kuwaambia watu mipango au malengo yako bali waoneshe watu matokeo. Washangaze watu kwa makubwa unayofanya na hiyo ndiyo heshima yenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; kuanzia leo chukua hatua na tekeleza kile ulichopanga kufanya. Waoneshe watu kile ulichofanya na usiwaoneshe watu mipango uliyopanga.
Kwahiyo, tunapojituma kuonesha matokeo ndiyo tunaweza kufanikiwa kwenye mambo mengi. Tuwe mabingwa wa kuonesha matokeo na tuwashangaze watu kwa yale tunayofanya.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.