Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sehemu Pekee Ambayo Unapaswa Kuweka Nguvu Zako Ili Upate Mafanikio

Rafiki,

Kuna vitu viwili muda na nguvu. Unaweza ukawa mzee una muda wa kutosha lakini huna nguvu ya kufanya kazi. Hivyo basi, tunatakiwa kulinda sana nguvu zetu sasa, maisha yetu yawe bora tunatakiwa kutumia nguvu zetu vizuri na kuzielekeza sehemu sahihi na siyo vinginevyo.

Huwa tunakosea kitu kimoja, watu wengi wanatumia nguvu kutafuta mali na siyo kutumikia watu.

Ukitaka kufanikiwa usiweke nguvu katika kutafuta mali, bali weka nguvu katika kutumikia watu na mali zitakuja zenyewe.

Mtu ambaye amejitoa kutumikia watu huwa anapata mali kirahisi, fanya kazi na mali na mafanikio ya kila aina yatakuja yenyewe hakuna uchawi. Usitegemee kupata mali kama hujaweka nguvu kuwatumikia watu.

Watu wako bize kutafuta mali badala ya kuwa bize kuwatumikia watu ndiyo waweze kupata mali. Tunatakiwa kuwawezesha wengine kuweza kupata kile wanachotaka na sisi tutapata kile tunachotaka katika maisha yetu. tunapokwenda kinyume basi, asili ya mafanikio huwa inakataa kabisa kutupatia sisi kile tunachotaka.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumika Kama Baraka Kuendeleza Dunia

Kama unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako, weka nguvu zako katika kutumikia watu na mali zitakuja zenyewe. Fanya kazi na mafanikio yatakuja yenyewe, usipende mafanikio kama hutaki kuwatumikia watu na kufanya kazi kwa sababu gani?

Chochote tunachokitafuta hapa duniani, tunakipata mikononi mwa watu hivyo usipojitoa kuwahudumia watu vizuri huwezi kupata kile unachotaka. Hebu niambie ni kitu gani ambacho unakitaka hapa duniani utaweza kukipata bila watu?

Hatua ya kuchukua leo; weka nguvu zako katika kuwatumikia watu na mafanikio yatakuja yenyewe.

Kwahiyo, hakuna mafanikio hapa duniani bila kuwatumikia watu, huwezi kupata mali kama huwatumikii watu. Watumikie watu na utapata kile unachotaka.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: