Design a site like this with WordPress.com
Get started

TAFAKARI YA JUMA LA 6 NA MAMBO KUMI NA MOJA NILIYOJIFUNZA

Mpendwa rafiki,

Hongera sana kwa kuwa na mwisho mzuri wa juma hili la sita. Natumaini yapo mengi uliyofanya na umepigwa hatua ukilinganisha na juma lililopita. Kama kila juma hupigi hatua maana yake unarudi nyuma.

Kumbuka maisha yana kwenda mbele na siyo  kurudi nyuma.

Katika kujitafari juma hili la sita nimejifunza mengi na sasa nakualika na wewe uweze kujifunza yale niliyojifunza mimi.

 1. Muda mwingine unashinda na muda mwingine unapoteza, huwezi kushinda kila siku.

Ni kweli sisi tumezaliwa kushinda, ila kwa asili ya dunia huwezi kuwa na hali moja muda wote, ndiyo maana kuna muda una kuwa hivi na muda mwingine vile. Tukielewa dhana hii kwamba hatuwezi kushinda kila wakati tutakuwa tunayopokea vizuri hata yale mabaya tunayokutana nayo. Kama leo ukishinda shukuru Mungu, kama ukikosa shukuru pia elewa kuwa asili ndivyo ilivyo huwezi ukashinda muda wote. You can’t win every time, sometimes you can win sometimes you can lose.

 1. Kwenye kila baya kuna zuri.

Tunapaswa kuelewa kuwa siyo kila changamoto ni laana kwetu, au kutuonesha sisi kuwa siyo wenye bahati. Amini kwamba kwenye kila baya huwa kuna zuri ndani yake. Kila baya linalotokea huwa linaambata na zuri ndani yake, kama hujui hilo chunguza utaona kwenye maisha yako.

 1. Huwezi kuwatawala watu.

Hakuna kazi ngumu sana kama kuongoza watu, kitu ambacho ni rahisi kuongoza ni kondoo, unaweza ukawaswaga kwenda sehemu moja lakini binadamu ni wagumu kufanya hivyo. Unaweza kumpa mtu kazi na ukategemea ataifanya na asiifanye hivyo  basi, chochote ambacho unampa mtu akufanyie jiandae na mawili tu, kufanikiwa au kuangushwa, kuwa tayari kupokea lolote, ukiwa ni mtu wa kujiandaa na kitu fulani na mambo yanapokwenda ndivyo sivyo lazima utaumia vibaya. Mtu ambaye hawezi kukuangusha ni wewe mwenyewe lakini usiweke mategemeo makubwa kwa watu wa nje kwani watakuangusha tu.

 1. Kama huna fedha huna tatizo unalotatua. Ukichunguza kwa makini msingi wa fedha ni kutoa thamani. Fedha haziwezi kukufuata hapo ulipo kama huna tatizo unalotatua. Mwalimu anatatua tatizo la ujinga ndiyo maana analipwa kadiri ya thamani yake, je kama huna tatizo unalotatua au thamani yoyote unayotoa je utalipwaje fedha.
 2. Mtu akiamua kuwahi anaweza. Kuwahi kwa mtu au kuchelewa kwa mtu eneo fulani ni maamuzi ya yule mtu. Watu huwa wanapima uzito wa tukio je linawasukuma kuwahi na wanaangalia je ni nani, wakijua ni mtu anayekwenda na muda hawatakuwa wazembe watafanya kila linalowezekana wafike mapema, hivyo binadamu wanajituma kadiri ya mtu asili ya tukio au mtu.
 3. Bila kuuliza hujifunzi. Mafanikio yanakwenda kwa wale wanaouliza na siyo wale wanaokaa kimya. Kuuliza siyo ujinga, hakuna mtu amezaliwa anajua yote hivyo usione aibu kuuliza kama hujui kitu, na unapouliza ndiyo unapunguza ujinga na usipouliza ndiyo unaongeza kiwango cha ujinga ndani yetu.
 4. Wivu ni hasara. Wivu umekuwa unawaumiza watu sana, kwanini fulani na siyo mimi, wengine wanapoona fulani amepiga hatua huwa wanaumia sana. watu wanapata hata magonjwa ambayo hayana hata vipimo hospitali yote haya ni kwa sababu ya wivu. Wivu ni kemikali mbaya sana ambayo inaweza kuu watu wengi sana kwa mara moja. Zipo njia za kujiondoa katika wivu lakini moja usijione wewe ndiyo una staili zaidi kuliko wengine. ukijiona wewe ndiyo unastahili zaidi kupata tu ukiwaona wengine wanapata roho itakuuma sana hivyo achilia yote, na ona kuwa kila mtu ana stahili kupata na huwezi kuzuia watu kuishi vile wanavyotaka.
 5. Mahusiano yanakufa. Mahusiano mengi kwa sasa yanakufa kwa sababu ya watu kutopeana muda. Uhai wa mahusiano ni muda,tumekuwa ni watu tunaishi hata nyumba moja lakini hatupeani muda kila mtu ana mambo yake. Tunapaswa kulinda mahusiano yetu kwa nguvu kubwa, kujenga mahusiano bora ni kazi hivyo usikubali kupoteza mahusiano yako bila kuwajulia hali na nini kinaendelea katika maisha yao.
 6. Ujasiria dini. Dini zimekuwa biashara, hivyo watu wamekuwa wanayumbishwa kiimani sana , wakitangatanga huku na huko wakitafuta miujiza ya haraka. Hivyo wanajikuta wanaliwa na kama msemo ule unavyodhirisha hili wajinga ndiyo waliwao. Huwezi kuamini kuna watu wanaigiza mambo ya kiimani ili wajipatie kipato, na chambo mkubwa amekuwa ni yule mtu ambaye hana mwelekeo, kwani ukikosa mwelekeo, basi mwelekeo wowote utakuchukua. Usitange tange kiimani, simama imara, usiwe Malaya wa kidini na linda imani yako. usijadanganye kushinda muda mwingi katika nyuma za ibada ndiyo kufanikiwa maisha. Hebu angalia tu wale waliofanikiwa wanafanya nini na wewe fanya, usisubiri muujiza, chukua hatua.
 7. Huwezi kuwa na uhuru wa kifedha kwa njia ya kuweka akiba tu. Katika jamii zetu kuna vikundi vingi vya kuchangishana fedha wengine wanaviita vikoba na majina mengine yanayohusiana na hayo. Tunapaswa kuweka akiba ili itusaidie kwa pale tunapopatwa na dharura lakini hupaswi kutumia njia moja ya kuweka akiba ili kukufisha kwenye uhuru wa kifedha. Unatakiwa kuwekeza halafu faida unayopata unaweka kwenye akiba. Unatakiwa kuwekeza zaidi, utakuta mtu ana tegemea mshahara halafu anakuambia atakua tajiri kwa njia tu ya kuweka akiba, utachelewa sana kufika lakini kwa kuizalisha ile fedha yako kwa kuwekeza maeneo tofauti tofauti utaweza kufikia mapema uhuru wa kifedha.
 8. Uongozi ni kama nyumba za kupangisha. Watu wanapoingia katika kuongoza watu hawajui kuwa kama ule uongozi wamepewa kwa muda tu, itafikia kipindi kodi yako itaisha na huwezi tena kuendelea kukaa pale.  Unapokuwa ndani ya kipindi cha mkataba wa uongozi wako jua kabisa umepewa uongozi kwa muda hivyo fanya kile unachopaswa kufanya na siyo vinginevyo. Usitumie matakwa yako kufanya kitu ambayo siyo sahihi. Kumbuka kama unamfanyia mtu ubaya na ubaya huo utakurudia tu hapa hapa duniani kabla hata hujafanya na hii ni kadiri ya sheria ya karma. Ambayo karma inasema kuwa chochote unachomfanyia mwingine malipo yake ni hapa duniani.

Kwahiyo, hayo ndiyo machache kati ya mengi niliyojifunza, mwisho wa juma hili ndiyo mwanzo mzuri wa juma linalokuja. Tukutane tena kwenye kipengele hiki juma lijalo la saba. Jenga utamaduni wa kila wiki wa kujitafakari kile unachofanya kama kina faida au la. Kwa sababu kama hujui unachofanya ni sawa na mtu anayechemsha mawe huku akisubiria yaive.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: