Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jambo Muhimu La Kufanya Katika Safari Ya Mafanikio Ili Ujisikie Raha

Mpendwa rafiki yangu,

Kila siku tunafanya kazi, tunakusanya fedha, tunapiga hatua moja kwenda nyingine hata umri wetu tulionao unabadilika kila siku. Kumbe mafanikio tunayopata kila siku ni makubwa sana katika safari ya mafanikio.

Kama leo uko mbele zaidi ya jana hayo nayo ni mafanikio. Nimeona watu wengi wamejikinai wao wenyewe dhidi ya maisha yao. Wanaona maisha yao hayana maana eti hawana kikubwa walichofanya katika maisha yao.

Katika watu waliokosa shukurani, basi sisi binadamu ni wa kwanza, hatuna shukrani kabisa, na katika maisha ya kiroho hata ya kawaida ukikosa kuwa na shukrani kwenye kila jambo basi utakua mtumwa wa kila jambo.

Rafiki, jambo muhimu la kufanya katika safari ya mafanikio ni kujipongeza kwa yale madogo au makubwa uliyofanya. Kujipongeza ni jambo muhimu sana ambalo kila mmoja wetu litamhamasisha kufanya kwa ubora zaidi. Usipokuwa mtu wa kujipongeza utachoka mapema, kazi tunazofanya zinachosha ila ukiwa unajipongeza ni kama unaongeza nguvu.

Mtu aliyejipongeza na kupongezwa kwa makubwa anayofanya au anayoendelea kufanya ni kama vile unazalisha kemikali ndani ya mwili wako ya kufanya mazuri. Muda mwingine tunaonekana hata kuchakaa katika maisha yetu ili hali tuna kila kitu, hii ni kwa sababu ya kutojipongeza na kukosa shukrani.

Tumeikabidhi furaha yetu katika vitu, endapo tutavikosa basi maisha yetu yanakuwa ya kinyonge sana. tumekuwa siyo watu wa kupongeza wala hata kujipongeza sisi wenyewe.

SOMA; Ujumbe Muhimu Kwako Kutoka Kwa Bilionea Richard Branson

Jikubali kwa hayo uliyofanya na jipongeze kwa zawadi nzuri, hata kwa kujinunulia kile kitu unachopenda. Umekuwa ni mtu wa kuwanunulia wengine zawadi na kuwapongeza wengine lakini wewe mwenyewe hujawahi kufanya hivyo.

Maisha yetu yanakuwa ya kimasikini kama tukikosa kuwa na shukrani na kutojipongeza kwa hatua kubwa au ndogo tunazopiga.

Hatua ya kuchukua leo; jipongeze kwa madogo au makubwa unayofanya au unayoendelea kufanya. Usisubiri mpaka watu wakupongeze jipongeze mwenyewe ili uzidi kufanya makubwa zaidi kwenye kile unachofanya.

Kwahiyo, ukishindwa katika madogo hata makubwa utashindwa. Msingi wa mambo yote unaanza na kuthamini kitu kidogo, hebu jifunze sasa kujipongeza kila siku kwa hatua unazopiga kwenye maisha yako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: