Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Husemwi Katika Maisha Yako, Basi Hufanyi Kitu Hiki Hapa Kimoja

Rafiki yangu mpendwa,

Hakuna mtu ambaye ana akili zake timamu ataweza kwenda kumpiga teke mbwa aliyekufa. Itakuwa ni jambo la ajabu sana.

Hakuna mtu mwenye akili timamu pia, atakwenda kurusha mawe kwenye mti ambao hauna matunda. Ukichukua mti wa mwembe ukaenda ukauweka katika ya shule ya msingi na ukachukua mti ambao hauna matunda ukaenda ukaweka katika ya shule ya msingi unafikiri wanafunzi watakimbilia mti gani ? jibu ni mti wenye matunda.

Kwa mifano hiyo hapo juu, inatosha kudhihirisha kuwa kama huna kumbwa unalofanya hakuna mtu atakaye kupiga vita, lakini kama unafanya mambo makubwa, unapiga hatua lazima watu watakupiga mawe, yaani watakupinga kwenye kile unachofanya.

Na hivi umeshawahi kujiuliza kwanini mtu ulipokuwa kawaida tu mlikuwa vizuri lakini baada tu yaw ewe kubadilika akaanza kukupinga? Hii ni kwa sababu anataka na yeye asionekane mzembe hivyo anakazana kukuangusha ili muonekane wote sawa. Kitendo tu cha wewe kupiga hatua kwake yeye ataonekana ni mzembe hivyo lazima atatafuta mbinu yoyote kukuangusha chini.

SOMA; Kama Unapitia Changamoto Yoyote Ile Usiache Kusoma Hapa

Hivyo basi, kama hupati changamoto basi huna kubwa unalofanya katika maisha yako. unafanya kitu cha kawaida sana ambacho kila mtu anaweza kufanya. Lakini ukienda hatua ya ziada lazima utakutana na upinzani mkubwa kwenye maisha yako.

Watu hawawezi kupoteza muda wao kuangaika na mtu ambaye hana madhara bali watu wanakwenda kuwasumbua  wale watu wanaopiga hatua kwenye maisha yao.

Hatua ya kuchukua leo; kama unakutana na changamoto , watu wanakupinga na kukusema basi ni dalili nzuri kuwa kuna kitu kikubwa unafanya cha tofauti ndiyo maana unapingwa hivyo endelea kufanya.

Kwahiyo, kama huna kikubwa unachofanya au unafanya kitu cha kawaida sana watu hawatakusumbua kwa sababu huna madhara, watu wanakuwa na nguvu kwenye vitu vikubwa na siyo vidogo.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: