Kama tunavyojua kuwa msingi wa fedha duniani ni kutoa thamani. Hivyo basi,
Tusitegemee kupata fedha kama hakuna thamani yoyote tuliyopanga kuitoa.
Kila mmoja wetu anamiliki kiwango cha fedha kadiri ya aina ya matatizo anayotatua kila siku. Kwa mfano, mwalimu anatatua tatizo la ujinga, askari anatatua tatizo la usalama. Je wewe unatatua tatizo gani ili uweze kulipwa?
Zawadi ya matatizo unayotatua ndiyo hukuletea fedha. Hivyo basi;
Fedha ni matokeo ya matatizo unayotatua. Kama unataka kupata fedha angalia matatizo ya watu na yatatue bila kufanya hivyo mambo hayawezi kwenda vizuri.
Kila siku utaendelea kupata kiasi cha kile kile mpaka pale utakapoamua kutoa thamani zaidi. Utakapoamua kutatua matatizo ya watu zaidi.
Kila mtu unayekutana naye , ni fursa kwako kuweza kufanikiwa. Hebu angalia unaweza kutatua shida gani ya watu katika eneo ulilopo na ukalipwa? Kaa chini na fikiria namna unanvyoweza kutafuta changamoto za watu ili uweze kufanikiwa.
SOMA; Kama Unataka Kiasi Kikubwa Cha Fedha, Badili Kwanza Kitu Hiki
Mafanikio tunayotaka yako mikononi mwa watu. Huwezi kupata chochote kutoka kwa watu kama hujawasaidia wao kupata kile wanachokitaka. Msingi wa mafanikio ni nipe nikupe, lakini kama ni wa kupokea tu, utaishia hapo hapo ulipo.
Toa zaidi, ili uweze kupokea zaidi, kuna matatizo mengi, jaribu kufiria namna ya kuja na suluhisho ili uweze kufanikiwa.
Hatua ya kuchukua leo; usilalamike huna fedha, bali lalamika kwa sababu hujatatua changamoto za watu au hujatoa thamani kwa watu, hujawawezesha watu kupata kile wanachotaka. Wasaidie watu leo ili uweze kulipwa.
Kwahiyo, usitegemee kufanikiwa bila kutatua shida za watu wengi, matajiri tunaowaona leo wamechagua kutatua matatizo makubwa ya watu. Kadiri unavyotatua matatizo ya watu wengi ndivyo unavyofanikiwa kifedha.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.