Mpendwa rafiki,
Natumaini unapoamka asubuhi tu salama kabla hujaenda kwenye shughuli zako huwezi ukasema leo ninakwenda kutafuta kushindwa, bali utasema leo nakwenda kutafuta ushindi. Kumbe basi, kadiri ya kila mtu huwa anatafuta ushindi ulipo.
Iko njia rahisi sana ya wewe kupata ushindi kwenye kile unachotaka, tunakosa ushindi kwenye kile tunachotaka kwa kukosa njia sahihi ya kupita. Siku zote ukipita njia sahihi huwezi kufika kule unakotaka kwenda.
Jinsi ya kupata ushindi kwenye kile unachotaka ni kufikiria kile unachotaka muda wote kwa kuiambia akili yako. kuna akili inayoitwa subconscious mind, yaani akili isiyokuwa na utambuzi, hii ni akili ambayo ikisikia jambo fulani basi itakomaa mpaka kuhakikisha inakupeleka kwenye kile unachotaka.
Hakuna kitu kibaya sana kwenye akili badala ya wewe kufikiria kile unachotaka, unaanza kufikiria kile usichotaka. Ni sawa na unataka kuwasha moto na kuuzima wakati huo huo je kwa namna hiyo utaweza kupata kile unachotaka?
Usiharibu siku yako, wiki, mwaka, mwezi au ndoto yako kwa ujumla kwa kufikiria kile usichotaka kwenye siku zote fikiria kile unachotaka ndiyo utaweza kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.
SOMA; KITABU; JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MABADILIKO 250 YA USHINDI
Kama unataka kufanikiwa basi fikiria kile unachotaka rafiki na siyo kile ambacho hukitaki. Akili huwa inakupa kile unachofikiria muda wote. Utapokea kadiri ya kile unachofikiria.
Hatua ya kuchukua leo; usifikiria yale ambayo huyataki katika maisha yako, bali fikiria kile ambacho unakitaka katika maisha yako.
Kwahiyo, dunia huwa inakupa ushindi unaotaka kama ukiwa king’ang’anizi kwenye kile unachotaka. Kwa kufikiria kile unachotaka na siyo kile usichotaka. Usivuruge mambo kwa kufikiria kile ambacho hukitaki kwenye maisha yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.