Rafiki,
Kila mmoja wetu anapenda mafanikio katika maisha yake. Ambaye hapendi mafanikio basi huenda hayuko katika sayari hii ya dunia. Kila siku tunaweka juhudi za kuwa bora katika maisha yetu ili tuweze kuwa na mafanikio kwenye kila eneo la maisha yetu.
Tunapambana usiku na mchana kutafuta mafanikio, kutafuta ubora, tunaenda semina, tuko katika program maalumu za kupatiwa mafunzo, tunasoma vitabu yote haya ni kuwa bora kila siku.
Kwahiyo, kila siku tunatakiwa kuwa bora zaidi ya jana. Je ni kitu gani kinachoweza kututoa hapa sisi tuliko na kwenda kule tunakotaka kwenda?
Kama kila mwezi huendi mbele basi jibu sahihi ni kuwa unarudi nyuma. Kama kuna sehemu huendi mbele basi jua kabisa unarudi nyuma kwa sababu katika maisha yako kuna mawili. Kwenda mbele na kurudi nyuma hakuna kusimama. Sijawahi kumsikia mtu akisema leo mimi ninasimama kuishi nitaanza kuishi mpaka siku fulani. Kama moyo wako unafanya kazi kila siku basi wewe uko katika mwendo na utakua hauko kwenye mwendo mpaka pale moyo wako utakaposimama na safari ya maisha yako itakuwa imeishia hapo.
Kitu pekee kitakachokupa mafanikio makubwa kwenye maisha yako siyo kitu kingine bali ni KUCHUKUA HATUA SAHIHI. Kama kweli unajifunza kila siku kwanini maisha yako hayabadiliki? Ni nini kinakufanya unarudi nyuma badala ya kwenda mbele? Unaona uchungu pale unaporudi nyuma na weka juhudi kuwa katika nafasi nzuri, usipende nafasi ya mwisho, kumbuka kama wewe siyo wa kwanza basi ni wa mwisho.
SOMA; Hii Ndiyo Siku Ya Bahati Katika Maisha Yako
Hufanikiwi kwa sababu huchukui hatua sahihi. Dunia huwa inampa ushindi mtu yeyote anayekuwa anachukua hatua sahihi. Na mtu akichukua hatua sahihi kwa kile anachojifunza basi huwa habaki kama alivyo lazima tu atafanikiwa.
Kama leo hii ukiamua kuchukua hatua sahihi katika maisha yako, mwezi ujao hutakua kama leo ulivyo. Huna haja ya kulalamika, wewe ni mtu mwenye bahati sana na bahati yako iko pale kama utachukua hatua.
Mafaniko uliyonayo sasa ni kwa sababu ulichukua hatua sahihi, kama unataka mafanikio yoyote yale, chukua hatua sahihi kadiri ya kile unachotaka.
Hatua ya kuchukua leo; kama uko katika maisha ambayo hayakulipi chukua hatua sahihi leo. Umeumbwa kuja kufurahia mema ya nchi, sasa kwa hali ya kutofanikiwa utafurahiaje mema ya nchi kama siyo kupata mateso?
Kwahiyo, kila mtu anaweza kuwa vile anavyotaka kuwa kadiri ya hatua sahihi atakazochukua katika maisha yake. Hakuna muujiza mwingine wa kupata mafanikio zaidi ya kuchuku hatua sahihi, kama unapanda mbegu kwenye mawe usitegemee hapo mbegu kuota, panda mbegu sehemu sahihi na utaona maajabu yatakavyotokea katika maisha yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.