Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Cheti Kikuu Kuliko Vyote Duniani

Mpendwa rafiki yangu,

Huwa sisi binadamu tunapenda pale tunaposoma, kuwekeza, kufunga ndoa, kufanya kitu fulani tupewe cheti kama cha uthibitisho fulani. Ndiyo maana ukiwa na soma mafunzo yoyote unatamani sana umalize na upewe cheti chako mapema na hata ukienda kuomba kazi unaonesha cheti cha kuthibitisha kuwa wewe umehitimu mafunzo fulani.

Tumekuwa ni watu wa kutafuta vyeti vilivyoandikwa kwenye makaratasi. Tumesahau kuwa tunacheti kikuu ambacho kinabeba vyeti vyote ambavyo tumewahi kuwa navyo. Cheti hicho siyo cheti kingine bali ni ubongo wako.

Ubungo wako ndiyo cheti kikuu kinachobeba kila aina ya mafunzo unayopata duniani. Unatakiwa kila siku kuboresha cheti chako ambacho ndiyo ubongo wako. Lisha maarifa chanya ili kiendelee kuwa na afya bora. Kama ubongo ukilala basi na mwili utalala, akili ndiyo imebeba kila kitu hivyo tutumie vizuri bongo zetu.

Usiwe mtu wa kuringa na cheti cha kwenye karatasi bali cheti kikuu kipo kwenye ubongo, unaweza kuwa vizuri kwenye cheti cha makaratasi kinaonesha lakini kwenye utendaji au ndani ya ubongo hakuna kitu. hivyo basi tunatakiwa tuwe ni watu wa kupenda kujifunza kila siku kufanya ubongo wetu uweze kwenda na wakati yaani update your brain.

SOMA; Uchambuzi wa kitabu; Philosophy of Happiness( Falsafa Ya Furaha)

Isafishe akili yako kama vile unavyosafisha mwili wako kila siku. Hujawahi kuondoka nyumbani ukiwa mchafu, umetoka hujapiga hata mswaki lakini ni rahisi kila siku kutoka nyumbani huku ukiwa hujaisafisha au kuulisha akili yako kitu chochote yaani maarifa chanya.

Ipende akili yako, kwani ubongo wako ndiyo mama wa mafanikio yote duniani. Safisha cheti chako kila siku ili uweze kuwa bora.

Hatua ya kuchukua leo; soma, jifunze sana ili kukisafisha cheti chako. Linda sana cheti chako kwani hakuna mtu mwenye cheti bora kama chako.

Kwahiyo, hiki ni cheti muhimu ambacho huwezi kwenda kukipata mahali pengine popote pale. Ubongo wako ndiyo sehemu pekee ambayo unaweza kupata kile unachotaka.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: