Design a site like this with WordPress.com
Get started

Punguza Matumizi Haya Ya Kifedha Ili Uweze Kufanikiwa Kiuchumi

Mpendwa rafiki yangu,

Bado suala la nidhamu ya fedha imekuwa ni tatizo miongoni mwa watu wengi. Hata uwe mtu unayepata kipato kikubwa kiasi gani na ukawa unatumia zaidi ya kile unachopata bado wewe ni masikini mkubwa.

Watu wamekuwa ni watu wa kutumia kile walichopata mpaka kiishe kwanza. Hakuna falsafa mbaya kwenye matumizi ya fedha kama tumia sasa na maisha ni sasa. Unajikuta unatumia halafu kesho itajijua yenyewe na ikifika kesho unaanza kupata shida na kukosa hata hela ya kula.

BONYEZA HAPA KUPATA KITABU HIKI CHA FUNGA NDOA NA UTAJIRI. KUPATA VITABU VINGINE VIZURI BONYEZA HAPA. KARIBU SANA RAFIKI

Kuna matumizi ya aina mbili;

Ya kwanza matumizi muhimu yaani haya usipofanya matumizi hayo basi maisha yako hayaendi. Ni matumizi muhimu sana kiasi kwamba tusipokuwa nayo maisha yetu hayawezi kwenda.

Ya pili ni matumizi yasiyo ya ulazima, yaani hata usiponunua maisha yako hayaathiriki kwa kitu chochote kile. Haya ndiyo matumizi mabaya ambayo yanawapelekea watu wengi katika umasikini na madeni yasiyokuwa na ulazima.

Wengi wanajikuta wako katika madeni ya vitu ambavyo havizalishi kabisa na baadaye wanakuja kujuta katika kulipa. Tumekuwa ni watu wa kununua vitu ili kuwafurahisha watu wasiojali.

Hakuna mtu anayejali juu ya maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe, hivyo kama unatumia ili uwafurahishe watu jua unajiloga wewe mwenyewe.

SOMA; Changamoto Zote Za Matumizi Ya Kifedha Zinaanzia Hapa

Leo rafiki nataka nikuambie kitu kimoja acha yale matumizi ambayo siyo muhimu yale ambayo unajisikia tu kununua lakini siyo muhimu. Unajua kuna watu wakiwa na fedha ni kama vile wanawashwa, wanataka dunia nzima ijue kama ana hela hivyo analazimika kutumia zaidi ili apate sifa.

Sifa nzuri ya fedha ni kuzalisha zaidi na siyo kutumia zaidi. Unatakiwa tu ujiulize hivi hawa waliofanikiwa kifedha wangekuwa ni watu wakutumia vile wanavyotaka bila kuwa na nidhamu ya fedha wangefika pale walipo?

Ukitaka kuishi maisha bora, anza kujikatalia mambo ambayo siyo muhimu kwako na uweke nguvu kwenye vitu bora kwako.

Hatua ya kuchukua leo; fanya matumizi yale muhimu tu, ambayo ukiyakosa maisha yako hayawezi kwenda. jiepushe na matumizi ya kujisikia kufanya hata kama siyo muhimu.

Kwahiyo, maisha yako yanahitaji uwe na nidhamu ya fedha. Msingi wa fedha ni kutoa thamani zaidi, toa thamani ili kuongeza kipato lakini pia tumia kiasi pale unapopata. Jiwekee msingi wa kiasi kwenye maisha yako.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana.

 

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: