Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Bora Ya Kujiandaa Kifedha Ili Kukabiliana Na Matukio Na Sikukuu Za Mwisho Wa Mwaka

Mpendwa rafiki yangu,

Dunia huwa inatupa kalenda ya matukio ya karibu mwaka mzima. Hapo ulipo tayari umeshakuwa na kalenda yako na unajua tukio fulani ni lini au siku gani. Hivyo, kama umeshakuwa na utambuzi huo unatakiwa sasa uchukua hatua ya kujiandaa kukabiliana na hayo.

Mwezi unaongozwa kwa matumizi makubwa huwa ni mwezi wa mwisho wa mwaka ambao ni wa kumi na mbili. Kuna kuwa na matukio mengi ya sherehe yanayohitaji fedha. Watu huwa wanatumia sana, wengine mpaka wanaishiwa na kupelekea wanadaiwa.

Kutokana na kuwa na matumizi makubwa inawafanya watu wengi kuingia mwaka mpya wakiwa wako vibaya katika eneo la fedha. Watu wanakuwa wanakabiliwa na njaa ya fedha ya kufanya vitu vingi, wengine wanatakiwa kulipia ada za watoto na kufanya malipo mbalimbali ya bili.

Nilikutana na mzee mmoja anasema anachukia kweli mwezi wa kwanza kwani Januari kwake inakuwa ni chungu kwa sababu anasomesha watoto wa nne na anatakiwa wote kuwalipia ada.

Unatakiwa sasa kujiaandaa na yote haya, jiandae kifedha kwa kutenga mafungu ya matukio hayo mapema kuanzia mwezi huu. Anza kutenga fedha kidogo kidogo kwa kujiwekea akiba yako pembeni ya kusherekea misimu yote ya sikukuu za mwaka ili inapokuja wewe huna tena mawazo sijui nitapata wapi fedha ya kufanya kitu fulani badala yake unachukua tu katika akiba uliyojiwekea na namna hii itakusaidia kukupa nidhamu ya fedha na kutokimbilia kukopa.

SOMA; Jinsi Ya Kukabiliana Na Madeni Katika Biashara Na Huduma Nyingine

Kama unasomesha anza kutenga fungu kila mwezi la ada ya mwakani, fungulia hata akaunti inapofika mwisho wa mwaka unakua huna mawazo ya kulipia ada.

Tuna bili nyingi za kulipia dawa ni kujiandaa mapema na kiasi hicho cha fedha tunachotakiwa kukitoa. Kipindi hiki fanya kazi sana, ongeza thamani ili upate fedha zaidi, kama una kipato kimoja ongeza zaidi.

Huwezi kuwa na uhuru wa kifedha kwa kuwa na chanzo kimoja cha mapato. Kuwa na mifereji mingi na fedha hazitokauka kwako.

Usiishi bila kuweka akiba,mtu makini anajiwekea akiba hata akipata dharura ya ghafla anakimbilia kwenye mfuko wake na siyo kwenye kukopa.

Hatua ya kuchukua leo; tenga mafungu ya  fedha unazopaswa kuzilipia hapo baadaye. Jiandae mapema usisubiri mpaka matukio yafikie ndiyo ujiandae wakati unajua kwa sasa unatakiwa kufanya nini.

Hivyo basi, maisha ni kujiandaa kukabiliana na ya sasa na yajao. Usiishi kama mnyama bali ishi kama binadamu aaliyepewa akili inayompa hekima, busara na utu. Jitambue na uchukue hatua.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: