Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Kitu Kinachoshindikana Kwa Mtu Huyu

Mpendwa rafiki,

Huwa tunasababu nyingi sana pale tunapotaka kuanza kufanya kitu, binadamu wamekuwa ni watu wa sababu kwanini hawezi na siyo kwanini wanaweza. Huwa tunajionea huruma sana katika maisha kwa kukimbia kazi na kuchagua kufanya vile vitu rahisi.

Asili ya kila binadamu ni kazi, binadamu ambaye hataki kazi hana sifa za kuwa binadamu. Huwezi kuishi bila kufanya kazi, maisha yetu ni kazi, kila siku ni mwendo tu, binadamu ni mtu wa mwendo na siyo mtu wa kukaa mahali pamoja.

Nikuambie tu kitu rafiki,

Hakuna mafanikio au kitu kinachoshindikana kwa yule mtu aliyeamua kufanya na yuko tayari kufanikiwa. Unaweza kuamua unataka kuwa mtu fulani lakini hujawa tayari. Hivyo unapokuwa tayari unakuwa umejipa kinga ya uthubutu ya kukabiliana na chochote kile utakachokutana nacho mbele yako haijalishi ni nini, bali wewe utajali matokeo tu.

Watu walioamua na kuwa tayari kufanikiwa wanaingia mazima, wanaingia kwa miguu yote, liwalo na liwe, vyovyote itakavyokuwa, wanaamua kujitosa kwenye maji, wanaaumua kujitoa usadaka kwa ajili ya kitu fulani.

Huwezi kusema wewe unataka kuwa mtu fulani halafu hauko tayari kulipia gharama, tunaona mifano mingi ya watu wa kale, wameweza kuwa mashujaa  kwa sababu waliamua na wakawa tayari kuwa vile wanavyotaka kuwa.

SOMA; Fanya Uamuzi Huu Wa Makusudi Kabisa Katika Maisha Yako

Maisha ni kuamua vile unavyotaka kuwa, ukiamua kuwa tajiri unaweza kuwa tajiri na hata ukiamua kuwa masikini unaweza kuwa masikini.

Kumbuka hali uliyonayo sasa umeamua kuwa na uko tayari kuishi hivyo, kama hali uliyonayo huipendi pambana kama vile mtu anayetafuta pumzi. Hutoangaiska kujishughulisha na kitu kingine zaidi ya pumzi unayotaka na kwenye mafanikio ndiyo hivyo ilivyo.

Hatua ya kuchukua leo; hakuna kitu kinachoshindaka kama ukiamua na ukiwa tayari kuw vile unavyotaka kuwa. Acha sababu, fanya kazi unayopaswa kufanya.

Kwahiyo, sababu huwa hazileti maendeleo kwenye maeneo ya maisha yetu, lakini kazi huwa inafanya maeneo ya maisha yetu kuwa bora sana.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: