Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hawa Ndiyo Watu Wanaohamasisha Watu

Mpendwa mwanamafanikio,

Hakuna mtu anayehamasika na mtu ambaye anafanya mambo madogo au anahamasika kwa mtu aliyefeli. Tulishajifunza kuwa unatakiwa kujifunza sana katika yale uliyofanikiwa na siyo yale uliyoshindwa.

Dunia huwa inapenda kuhamasika na watu wanaofanya makubwa, watu wenye maono makubwa ambao wamechukua hatua kubwa.

Watu wanapenda kufanya kazi au kumfuata mtu anayewahamasisha kwa kitu fulani,na mara nyingi watu wanapenda kujihusisha na mtu anayefanya makubwa kushinda yeye ili ahamasike nay eye.

Kama tunavyojua maisha yetu yamebebwa na hamasa hivyo kama hatuna ndoto inayotupa hamasa hakika hatutoweza kuhamasika.

Malengo yetu ndiyo yamebeba ndoto zinazotupa hamasa, kama ndoto yako ni ndogo wala haitokupa hamasa ya kufanya kwa hatua ya ziada, utaridhika sana. kuwa na ndoto kubwa , malengo makubwa ambayo watu wakiyasikia watasema hayawezekani kutokea.

Tafuta watu wanaokupa hamasa lakini na wewe ujitoe usadaka kupata kile unachotaka, ni rahisi kuhamasika juu ya mtu au kitu fulani lakini kwenye kuchukua hatua kuna maumivu makubwa.

Waswahili wanasema ukiona vya elea ujue vimeundwa, kila kitu unachokiona jua kabisa watu wamefanyia kazi juu ya kitu hicho.

SOMA; Hii ndiyo Hamasa Kwa Mtu Aliyekata tamaa Hapa Duniani

Badala ya kujikumbatia na kujiona huruma kubali kujitoa usadaka , kumbuka hata unajipenda kiasi gani lakini hakuna upendo bila kujitoa. Angalia watu wote wenye upendo wamejitoa kwa kitu fulani je wewe umejitoa kwa kitu gani?

Hatua ya kuchukua leo, kuwa na malengo au ndoto kubwa zinazokupa hamasa, kuwa na watu wa mfano watakaokuhamasiaha. Lakini pia, ujiandae kujitoa usadaka kupitia kile unachotaka kufanya.

Kwahiyo, chukua hatua ili ndoto zako zitokee katiika hali ya uhalisia au lala nazo, uendelee kuota kila siku, maamuzi ni yako, amua kile unachotaka na kifanyiekazi.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: