Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hili Ndiyo Eneo Lenye Utajiri,Fedha Na Mafanikio Makubwa

Rafiki,

Kama umeamka na hujui nini unatakiwa kwenda kufanya rudi kitandani ukalale. Hivi mpaka leo hii kuna mtu bado hajajua kusudi la maisha yake? Kama bado hujajua kusudi la maisha yako basi nakusihii sana usome kitabu kinachoitwa ONGEA LUGHA YAKO, SAUTI YAKO YA NDANI NDIYO MAFANIKIO YAKO.  Hivyo kuwa huru kuwasiliana na mimi ili uweze kujipatia nakala yako.

Tusipojijua tuna nini ndani yetu na kujitumia vizuri mwisho wa siku tutanuka. Kama hufanyi kazi na huna kusudi unalofanya hapa duniani basi utanuka kwa sababu kupitia kazi  na kile anachopenda mtu ndiyo kusudi la mtu lipo.

Huwa tunafuta utajiri,mali na mafanikio makubwa lakini watu wengi bado hawajajua eneo lenye utajiri na mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.  Kwahiyo,

Eneo lenye utajari na mafanikio makubwa siyo lingine bali ni kusaidia au kutoa kwa  ajili ya  wengine . Chochote ambacho unachotaka sasa kinapatikana kwa watu. Kama ndoto yako ni kuwa na gari watu ndiyo wanatengeneza hilo gari hivyo ukiwa unataka chochote katika hii dunia kinapatikana kupitia binadamu.

SOMA; Njia ya uhakika ya kupata mafanikio makubwa

Hata kama wewe ni muombaji mzuri, unasema hutegemei watu lakini kupitia kile unachoomba kwa Mungu  atajimwilisha kwa watu na wewe utapata kile unachotaka. Mungu hawezi kushuka bali atajimwilisha kupitia watu ambao tuko nao hapa duniani. Changamoto au kile unachotaka kinatatuliwa na watu.

Hivyo basi,

Hakuna rasilimali muhimu kama watu. Watu ndiyo watakusaidia kupata kile unachotaka katika maisha yako.

Eneo lenye utajri kuliko yote ni kujitoa kwa ajili yaw engine. Ni heri kutoa zaidi kuliko kupokea zaidi.  Kuna watu kazi yako wao ni kupokea tu ndiyo maana hawafanikiwi, lakini kuwa mtoaji na mafanikio yatakuja yenyewe. Kama unataka fedha toa thamani kwa wengine, jali maslahi yaw engine, yaweke mbele, watatulie shida zao halafu na wewe utapata kile unachotaka.

Nina amini na ninalifanyia kazi kila siku, fedha , utajiri na mafanikio ni haki yetu na viko na vinapatikana kama tukikubali kujitoa kwa ajili yaw engine.

Wasaidie watu kwenye wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka ni hivyo tu. Hakuna uchawi , bali ni sayansi ya kupata utajiri na mafanikio makubwa.

Hatua ya kuchukua zaidi. Kama unataka chochote, basi toa zaidi, kama unataka fedha toa thamani zaidi kwa sababu msingi wa fedha ni kutaoa thamani kwa wengine na kadiri unavyotoa  thamani ndivyo unavyozidi kupata fedha nyingi na kufanikiwa.

Kwahiyo, unapojitoa na kusaidia wengine ndiyo Baraka na mafanikio makubwa yanakuja kwako. Kila litu tunachotaka kipo, dunia ina utele wa kila kitu, haina uhaba lakini utapata uhaba pale tu wewe utakappkuwa mchoyo wa kutoa, ila yule anayetoa anapokea zaidi. Angalia wengine wanataka nini, wasaidie na mafanikio yatakuja yenyewe.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: