Rafiki,
Najua unahitaji mafanikio, ila siri ya mafanikio iko wazi kabisa ni kuwawezesha wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka.
Ila watu shida yao moja ni kwamba hawataki kujitoa kwa ajili ya wengine hawajui kuwasaidia wengine ndiyo wao kufanikiwa.
Njia ya uhakika ya kupata mafanikio ni kuweka maslahi ya wengine mbele, toa thamani kubwa kwa kuhudumia watu wengi zaidi.
Ukijitoa kuwahudumia watu watakurudishia upendo wa kile ulichowapa. Njia ya uhakika ya kujitoa kupata mafanikio ni kuweka maslahi ya wengine mbele.
Leo nenda kajitoe kuwasaidia wengine ili waweze kupata kile wanachotaka katika maisha yao na wewe utapata kile unachotaka.
SOMA; Dalili Nzuri Ya Kuonesha Kuwa Unapiga Hatua Za Kimafanikio
Hatua ya kuchukua leo, wasaidie wengine kupata kile wanachota na wewe utapata kile wanachotaka.
Hivyo basi, hii ndiyo njia ya uhakika kabisa ya kupata mafanikio makubwa ni kutoa thamani kubwa kwa wengine, kama hujitoi kwa wengine huwezi kupata kile unachotaka.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana